MWENYEKITI
wa Chadema, Freeman Mbowe aweonya kuwa chama chake kitawachukulia watu
wanatumiwa kutaka kukivuruga chama hicho huku akibainisha kwamba Chama chake
hakina mpasuko wala mgogoro wa aina yoyote.
Akizungumza
na wafuasi wa Chadema katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es
Salaam jana, Mbowe alisema chama hicho bado kipo imara na hakuna mpasuko kama
ambavyo imekuwa ikidaiwa.
Mbowe
alikuwa akizungumza na wafuasi hao ambao walifanya maadamano kutoka Mahakama ya
Rufani hadi ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni, baada ya kada wa chama
hicho, Godbless Lema kushinda rufaa yake iliyomrejeshea ubunge wa Arusha Mjini.
Mbowe
alisema wapo baadhi ya watu wanaotumiwa kutaka kukivuruga Chadema kwa kueleza
mambo yasiyo na ukweli lakini watambue kwamba Chadema hakiwezi kuyumbishwa na
maneno ya watu na kwamba hakina mpasuko wala mgogoro wowote kama inavyo daiwa.
“Kuna watu
wanasema kwamba Chadema kina mpasuko na mgogoro mkubwa lakini watu watambue
kwamba Chadema kipo imara na kwamba hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote yule
mwenye nia mbaya ya kutaka kuvuruga Chama,” alisema Mboye na kuongeza:
“Chama chetu
ni imara na kinachowajali wananchi na kwamba sisi hatuwezi kusikiliza
maneno ya watu wanaotaka kukivuruga chama kwa lengo la masilahi yao binafsi
kwani lengo letu ni moja kutaka kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wa
taifa hili.”
No comments:
Post a Comment