To Chat with me click here

Sunday, December 16, 2012

HATIMAYE MWILI WA MAREHEMU MARYSTELLA WAACHIWA HURU

Hatimaye  mwili wa marehemu, Marystella Alphonce, uliokuwa umezuiliwa katika Hospitali ya Hindu Mandal umekabidhiwa kwa ndugu zake baada ya kufikia makubalino ya malipo.

Mwanamke huyo alifariki Alhamisi wiki hii na kuacha deni la Sh. milioni 7.2 baada ya  matibabu kwa kutumia huduma ya bima ya afya iliyokuwa inamilikiwa na Honoratha Magezi.

Utata huo ulibainika baada ya ndugu wa marehemu kutaka kubadilisha jina katika hati ya kifo na kutaka liandikwe jina la Marystella badala ya jina la Honoratha ambalo alikuwa akitumia wakati alipokuwa amelazwa hospitalini hapo.

Afisa Utawala wa Hospitali hiyo alisema nasi, Juma Fundi, alisema mwili wa marehemu huyo ulichukuliwa majira ya saa 1 usiku  baada ya taratibu zilizotakiwa kufuatwa kukamilika.

Fundi alisema ndugu wa marehemu wameandikishiana mkataba kwamba watalipa fedha hizo kwa awamu mpaka watakapokamilisha deni hilo.

Alisema hawajatoa muda wa kumalizika kwa deni hilo kutokana na ndugu kuahidi wenyewe kulimaliza kwa awamu tofauti.
Fundi alisema Hospitali yake imeandaa mfumo mpya ambapo mgonjwa ataonyesha kadi yake kwa daktari anayemtibu ili kuondokana na matatizo kama hayo yaliyojitokeza ya mgonjwa kutumia kadi ya mtu mwingine.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto, alisema mpaka sasa mhusika wa kadi aliyokuwa anatumia marehemu hajajitokeza polisi licha ya mumewe Dk. Jovis Mugezi kuendelea kushikiliwa.

Mgonjwa huyo ambaye alilazwa hospitalini hapo tangu Novemba 12, mwaka huu baada ya kufariki ndipo ilipobainika kuwa alighushi kadi ya mtu na kujipatia matibabu kinyume na sheria.

No comments:

Post a Comment