MAENEO
YA KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI HIII,WATU WAWILI WAMEPOTEZA MAISHA NA
MMOJA KUJERUHIWA MGUUNI BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA GARI MOJA DOGO LILILOKUWA
LIMEBEBA HELA AMBAZO WALIKUWA WAKITAKA KUZIIBA.
MAJAMBAZI
HAO WALIFANIKIWA KUMUUA MMILIKI WA GARI HILO PAPO HAPO BAADA YA KUTOKEA
MALUMBANO, WAKATI WALIPOKUWA WAKITAKA KUFUNGULIWA GARI HILO HUKU YEYE AKIKATAA.
NA
WALIPOFANIKIWA KUCHUKUA HELA HIZO WAKAWA WANAKIMBIA HUKU WANANCHI WENYE HASIRA
WAKIWAKIMBIZA NA NDIPO MAJAMBAZI HAO WALIPOAMUA KUANZA KUPIGA RISASI HOVYO NA
KUMKUTA MTU MMOJA KICHWANI AMBAYE NAYE ALIPOTEZA MAISHA HAPOHAPO NA KUMJERUHI
MWINGINE MGUUNI.
JESHI
LA POLISI LILIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUANZA KUFUKUZANA NA MAJAMBAZI HAO, AMBAO
WALIFIKA SEHEMU NA KUZITEREKEZA HELA HIZO NA WAO KUINGIA MITINI.
JAMBAZI
MMOJA ALIKIMBILIA NDANI YA DUKA MOJA LA NGUO ZA NDANI MAENEO HAYO YA KARIAKOO
MTAA WA KONGO KWA LENGO LA KUJIFICHA ALITIWA MBARONI NA POLISI AKIWA NA BASTOLA
MOJA AMBAYO ALIKUWA AMEIFICHA DUKANI HUMO PAMOJA NA NGUO.
JAMBAZI
MWINGINE AMEUWAWA KATIKA MASHAMBULIO NA POLISI. HIVYO MPAKA MWANHABARI WETU
AKIONDOKA MAENEO YA TUKIO, POLISI WALIKUWA WAMEFANIKIWA KUKAMATA HUYO MMOJA NA
KUUA MWINGINE HUKU WAKIWA WAMEKAMATA BASTOLA MOJA.
No comments:
Post a Comment