WAKATI
Rais Jakaya Kikwete akiwaapisha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Aprili
13 mwaka huu alionya kuwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya usifanywe kwa kuegemea
udini, ukabila, ubinafsi, siasa ama kulenga kuvunja Muungano.
Anasema
maoni ya wananchi lazima yaheshimiwe hata kama hayataweza kuingizwa
yote katika katiba hiyo, huku akiwataka wajumbe hao kuweka pembeni maslahi ya
makundi wanayotoka kwa kuwa kazi wanayoifanya ni kwa maslahi ya taifa..
Tume
hiyo ilianza kazi yake ya miezi 18, Mei mosi mwaka huu, ambapo mpaka sasa
imeshakusanya maoni katika mikoa takribani 15.
Mbali
na kukusanya maoni ya wananchi na kutengeneza rasimu ya katiba, baadaye
zitafuata hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge Maalumu la
kuchambua rasimu hiyo, kisha wananchi kupiga kura ya maoni.
Tume
hiyo ya Katiba jana ndio imemaliza kukusanya maoni ya Wananchi na kuanza
kujipanga kwa taratibu nyingine za kumaliza kazi yake.
Pamoja
na maelezo hayo ya Rais Kikwete watu wa kada mbalimbali likiwemo Jukwaa la
Katiba Tanzania walipinga kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana Aprili 18, 2014
kama serikali inavyoeleza.
Wakipendekeza
kwamba ili Katiba iweze kutumika ni lazima sheria nyingine zirekebishwe, zoezi
ambalo huchukua miaka miwili.
Walisema
kinachotakiwa kufanyika ni kurekebishwa kwa Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa
katika vipengele vinavyohusiana na Tume ya Uchaguzi, ili uchaguzi wa mwaka 2015
uwe huru na wa haki, kuacha mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya
ukiendelea kwa utaratibu mzuri.
Hoja
hiyo ilinaonekana kuwagusa wengi na sasa, Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anasema jambo hilo linatakiwa
kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
“Chadema
tunaingiwa na hofu kwamba huenda Katiba mpya isiwe tayari kabla ya uchaguzi wa
Serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015” anasema Mbowe.
Anasema
hakuna ulazima wa kupatikana kwa Katiba mpya katika kipindi hicho, badala yake
mchakato huo uendelee lakini yafanyike marekebisho katika Sheria ya Uchaguzi ya
mwaka 1985 ambayo ndani yake kuna Tume ya Uchaguzi (Nec) na daftari la kudumu
la wapigakura.
“Kuna
mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi, kwanza ni kuwa na Tume huru ya Uchaguzi na
mchakato wa kupata tume hii ufanyike bila kuathiri mchakato mzima wa kupata
Katiba mpya.
No comments:
Post a Comment