To Chat with me click here

Monday, December 31, 2012

WEDDING ANNIVERSARY


Mr. & Mrs. Kattikiro Jr
Kawaida ifikapo kila 31 December ya kila mwaka, kila mmoja duniani kote hukumbuka au kusherehekea kumaliza mwaka na kuanza au kuukaribisha mwaka mwingine unaoanza saa 6 kamili usiku wa siku hiyo. Kwetu sisi kama familia ya Mr. & Mrs. Kattikiro Junior tumekuwa tukikumbuka juu ya tukio la muhimu sana kwenye maisha yetu, kwani siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita tuliweza kufunga ndoa takatifu katika kanisa kuu la Mt. joseph Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam. 

Kwakweli tumepitia mengi katika mwaka huu mmoja wa maisha ya ndoa, pamekuwa na magumu mengi, lakini vilevile pamekuwa na neema nyingi mno. Mbali tu na Challenges nyingi za kimaisha lakini tumekutwa na misukosuko mingi katika maisha yetu ya kifamilia. Lakini kwa neema za Mungu tumeweza kuendelea kushikamana na kuweza kujikwamua kutoka katika matatizo na magumu hayo.

Kwa namna ya pekee kabisa tunapenda kuwashukuru wote ambao wamekuwa msaada mkubwa kwetu tangu tulipopata wazo la kufunga ndoa na kulikamilisha kulingana na taratibu za imani yetu hadi kufika leo hii ambapo tunaadhimisha mwaka mmoja wa ndoa. 

Tunawashukuru ndugu zetu wote, familia zetu, majirani na marafiki zetu wote kwa mshikamano, upendo, na misaada yao ya hali na mali wakati tulipo ihitaji. Tunaomba mzidi kutusaidia na kutuombea ili tuweze kudumu katika maisha ya ndoa. 

Lakini zaidi ya yote, tunatoa shukurani zetu za pekee kabisa kwa Mwenyezi Mungu, Baba yetu wa mbinguni, kwakuwa yeye ndiye amekuwa kiongozi wa familia yetu, amejalia wingi wa neema zako mno, zaidi tunamshukuru kwa kutupatia zawadi ya mtoto wa kike (Maureen Maxmillian Kattikiro). Kwakweli Jina la Mungu lihimidiwe.

Mwisho kabisa napenda kuwatakia furaha ya mwaka huu mpya na Baraka tele za Mungu Mwenyezi ziwe juu yenu nyote, ili sote kwa pamoja tuanze mwaka huu kwa amani na imani ya kufanikiwa zaidi. 

HAPPY NEW YEAR 2013 !!


MR. & MRS. KATTIKIRO JR.
31st DECEMBER 2012

MBOWE AWAKUNA WATANZANIA


SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kutangaza kutogombea urais mwaka 2015 na kwamba badala yake anajielekeza kupanga na kutekeleza mikakati kuhakikisha chama chake kinaingia Ikulu, Watanzania wamemuunga mkono wakisema ni mkomavu kisiasa.

Mbowe alihutubia mkutano jimboni Karatu juzi na kusema kuwa kazi yake itakuwa kusimamia kupata viongozi bora wa kupeperusha bendera ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Kauli hiyo ya Mbowe ilimaliza uvumi uliokuwepo kuwa huenda angegombea, ila aliweka bayana kuwa mgombea wao wa mwaka 2010, Dk. Willibrod Slaa, bado anatosha kugombea wadhifa huo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya ya kuwapatia wabunge wengi.

Msimamo huo wa Mbowe, jana ulitawala katika mijadala ya wananchi kwenye mazungumzo ya kawaida na mitandao ya kijamii, huku wengi wakimuunga mkono na kudai si king’ang’anizi wa madaraka.

Wananchi hao katika mitandao ya kijamii walikwenda mbali zaidi wakiwataka hata viongozi wakuu wa vyama vingine vya upinzani, ambao wamewahi kuwania nafasi hiyo bila mafanikio makubwa, kutengeneza mkakati wa kuwaandaa wagombea wengine wanaokubalika zaidi yao.

Miongoni mwa viongozi waliotajwa kupoteza mvuto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, ambao wamegombea kiti hicho bila mafanikio mara nne mfululizo tangu mwaka 1995.

Akizungumza na Tanzania Daima, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alimpongeza Mbowe kwa hatua ya hiyo.
Dk. Bana alisema kuwa, Mbowe ameonesha ukomavu wa kutokuwa king’ang’anizi wa madaraka, jambo alilodai ni jema la kujipima mwenyewe na akatoa msimamo usiotiliwa shaka.

“Mbowe kwa sasa ni mwanasiasa pekee aliyeonesha upeo wa hali ya juu, na kweli anafaa kuwa kiongozi wa chama anachokiongoza, na tumemshuhudia akiongoza kwa ukomavu sio katika chama tu ila hata kambi rasmi ya upinzani bungeni,” alisema.

Aliongeza kuwa, kama anaweza aangalie wagombea mbalimbali kuwaandaa mapema na si kuwakurupua kama walivyofanya wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 kwa kumkurupua Dk. Slaa.

Naye mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Bashiru Ally, alisema kuwa CHADEMA kimeonesha mfano, na hivyo CCM waige kwani suala la mbio za urais kupitia CCM limekuwa ni vita hadi limetikisa nchi.

“Watu wamechafuliana majina, wanakamiana kisa urais. CCM wanaumwa ugonjwa wa kutaja majina badala ya sifa za wagombea, kila siku ukiwauliza kama wanagombea au hawatagombea, watu hujibu majibu ya mkato, subiri nitaoteshwa au huwezi kuvuka daraja kabla ya kulifikia,” alisema.

Alisisitiza kuwa, kweli wanampongeza Mbowe na sasa wanamshauri atengeneze mchakato wa wazi wa kupata mgombea ambaye ataungwa mkono na Watanzania wengi.

“CHADEMA sasa kinakua kwa kasi, haijulikani ni kwanini japo watu wengi wanahusisha na uungwaji mkono na vijana na wasomi mbalimbali, hivyo ni wakati wa kuwafunda vijana wake ili wajue sifa za uongozi,” alisema.

Bashiru alisisitiza kuwa, vijana wanapaswa kujulishwa kuwa ujana si sifa ya mtu kuwa rais, kwamba kuna sifa zaidi ya ujana zinahitajika.

Katika mchango wake kwenye mtandao wa kijamii, mhadhiri mwandamizi wa UDSM, Dk. Azavery Lwaitama alisema kuwa Mbowe ametoa kauli ya kumuunga mkono Dk. Slaa ambaye kura zake zilichakachuliwa mwaka 2010.

“Kwa Mbowe kusema kuwa hatakuwemo katika kinyang’anyiro cha kugombea urais ndani ya CHADEMA, hivi ndani ya CCM kungekuwa hakuna ukomo wa urais si ningekuwa  nasikia maoni kama haya kuwa mgombea wa 2010 ndiye huyo wa 2015?” alihoji.

Aliongeza kuwa, hivi karibuni wakati wa uchanguzi wa UVCCM ililazimishwa kuwa mwenyekiti atoke Zanzibar na kwamba vile vile kwa Spika Anne Makinda ililazimishwa ili kumwengua Samuel Sitta.

“Tumpongeze Mbowe kwa kuondoa ubinafsi na kumtangaza mwenzake kuwa anatosha kwani si alishinda 2010 bwana, lakini kura zikachakachuliwa na wale wale ambao wamekuwa wanapanga na kutekeleza mipango ya kishetani ya kumuua Dk. Slaa ili kuuzima umaarufu wake na kuisambaratisha CHADEMA,” alisema.

Dk. Lwaitama aliongeza kuwa, CCM kwenyewe tayari Januari Makamba ameishatangaza kuwa lazima mgombea awe kijana na kwamba hata Rais Jakaya Kikwete aliishatangaza kuwa atakapotoka anataka akabidhi urais kwa mtu mwenye umri mdogo kuliko yeye.

“Nadhani tuwaache CHADEMA wapeane maelekezo wao kwa wao. Na tumpongeze Mbowe kwa kutanguliza masilahi ya chama chake na taifa kwa ujumla badala ya masilahi ya kwake binafsi,” alisema.

Alifafanua kuwa, sasa propaganda za CCM kwamba Mbowe naye anautaka urais zimetunguliwa hivyo na labda sasa zitabaki za Zitto Kabwe kuusaka urais.

Kwamba ikitokea Zitto akatamka kama alivyotamka Mbowe, basi nazo zitapeperushwa na upepo zibaki sasa propaganda za kumchafua Dk. Slaa.

LEMA KUJITWISHA ZIGO LA MABILIONI YA USWISI


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amesema atamshawishi mbunge mwenzake wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ili ampatie majina ya vigogo walioficha fedha Uswisi awataje bungeni.

Zitto ndiye aliibua hoja hiyo bungeni na kuwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge liazimie kwa kauli moja na kuunda kamati teule ya kuchunguza tuhuma hizo na kuwachukulia hatua, vinginevyo serikali ikishindwa atawataja.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Kahama mkoani Shinyanga, alipopata mapokezi ya kifalme akiwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche na kada mwingine, James Ole Millya, alisema kuwa atataja majina hayo bungeni.

Lema alisema kuwa Watanzania wamekuwa na shauku ya kuwafahamu viongozi wao mafisadi waliopora fedha zao na kwenda kuzificha katika nchi za ughaibuni kama Uswisi, Mauritania, Dubai na Morocco.

Alisema tangu hoja hiyo ifikishwe bungeni na serikali kuahidi kufuatilia, hadi sasa kumekuwa na ukimya ambao unazua maswali juu ya ukweli wa suala hilo kutoka kwa wananchi.

“Nitamuomba Kamanda Zitto anipatie majina hayo nami Bunge lijalo niyaanike ili kukata kiu ya Watanzania walio na haja kubwa ya kuwafahamu, hata kama hatua hiyo itanisababishia kifo, mimi siogopi kufa,” alisema Lema.
Aliwataka wakazi wa Kahama kuondokana na woga pindi linapofikia suala la kupigania haki zao na akasema wasiwaachie viongozi na wanachama wa CHADEMA pekee.

Lema aliishutumu Serikali ya CCM akidai imeshindwa kuwajengea miundombinu mizuri na kuwakopesha mitaji mikubwa wachimbaji wadogowadogo pindi wanapovumbua maeneo yenye madini.

Alisema kuwatimua wachimbaji hao ni kupanua wigo wa watu wasiokuwa na ajira, ombwe ambalo linaweza kuigharimu nchi hata kuingia katika machafuko.

Wakati huo huo, kada mashuhuri wa CCM, Frank Mwaisumbe, aliyeitikisa ngome ya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 akiwania ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini, amehamia CHADEMA.

Mwaisumbe aliyewahi kuwa Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa, kabla ya kuachana na kazi hiyo, ametangaza kujiunga na CHADEMA juzi.

Alisema CCM imeshindwa kushughulikia kero na matatizo ya wananchi ikiwemo rushwa na makundi yanayowania madaraka.

Jimbo hilo la Mbeya Mjini kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu baada kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Benson Mpesya.

Katika hatua nyingine, vijana wametakiwa kutokuwa na fikra mgando katika kupambana na matumizi mabovu ya rasilimali yanayofanywa na baadhi ya watu wachache ili kuliokoa taifa linaloangamia.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Joseph Lyata katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Luganga wilayani Kilolo.

Lyata alisema ili taifa liweze kusonga mbele, lazima liwe na watu wenye uchungu na rasilimali zilizopo na kujali matumizi ya pamoja.

Happy New Year 2013



New Year is the time at which a new calendar year begins and the calendar's year count is incremented. In many cultures, the event is celebrated in some manner. The New Year of the Gregorian calendar, today in worldwide use, falls on 1 January, as was the case with the Roman calendar. There are numerous calendars that remain in regional use that calculate the New Year differently.

The order of months in the Roman calendar was January to December since King Numa Pompilius in about 700 BC, according to Plutarch and Macrobius. According to Catholic tradition, 1 January is the day of the circumcision of Jesus (on the eighth day from his birth), when the name of Jesus was given to him (Luke 2:21).

It was only relatively recently that 1 January again became the first day of the year in Western culture. Until 1751 in England and Wales (and all British dominions) the New Year started on 25 March – Lady Day, one of the four quarter days (the change to 1 January took place in 1600 in Scotland). Since then, 1 January has been the first day of the year.


Thus, for such a little understanding on New Year Event, Maxmillian Kattikiro  would deeply love to wish all our dearest viewers and followers of our blog the happiest moment and God’s blessings when we start the new calendar of the year 2013 in our lives. 

Stay blessed and keep on following Maxmillian Kattikiro Blog.

Blog Administrator,
Maxmillian Kattikiro.
31st December 2012.