Tume hiyo inayoundwa na watu 34 itaongozwa na Mwenyekiti wake Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu
Mstaafu Augustino Ramadhan, Katibu ni Assad Ahmed Rashid na Naibu Katibu
Casmir Sumba Kyuki.
Kuundwa kwa tume hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete aliyoitoa
Desemba 31 mwaka 2010 kwenye hotuba yake ya kuuaga mwaka ambapo alisema
atahakikisha hadi kufikia mwaka 2014, Tanzania itakuwa na Katiba Mpya
itakayokidhi matakwa ya Watanzania
Katika mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es
Salaam Rais Kikwete ameeleza namna tume hiyo ilivyoundwa kwa kuzingatia
pande mbili za Muungano.
Rais ameweka wazi majina ya wajumbe 15 wanaounda tume hiyo kutoka
Zanzibar kuwa ni Dokta Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha
Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussi Khamis Haji, Salma
Maoulidi, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Said, Muhammed Yussuf
Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed,
Abubakar Mohammed ALI na Ally Abdullah Ally SALEH.
Kwa upande wa wajumbe kutoka Tanzania Bara, Rais amewateua Profesa
Mwesiga Baregu, Riziki Shahari Mngwali, Dokta Edmund Adrian Sengodo
Mvungi, Richard Shadrack Lyimo, John Nkolo, Alhaj Said El- Maamry, Jesca
Sydney Mkuchu, Profesa Palamagamba Kabudi, Humphrey Polepole, Yahya
Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Malingumu Kashonda, Al-Shaymaa Kwegyir,
Mwantumu Jasmine Malale na Joseph Butiku.
Utata wa Wajumbe wa Kamati:
Rais akimwapisha Mhe. Al-Shaymaa Kwegyir, mbunge wa viti maalumu kuwa mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo. (Utata)
Rais akimwapisha mwakilishi toka baraza la uwakilishi - Zanzibar (Utata)
Hapa akimwapisha Prof. Mwesiga Baregu - Mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na Mkuu wa kampeni yake 2010Hapa anamwaipsha Dr. Sengodo Mvungi ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR Mageuzi
Je! kulingana na sheria, kuna uhalali wa watu hawa kuwa wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya Katiba mpya ikiwa sheria inakataza kabisa na waziwazi kuwa wabunge na wawakilishi au viongozi wa kisiasa wasiwe wajumbe wa Tume? Je, huu si mgongano wa Kimaslahi kwa hawa wajumbe wa Tume wenye Utata? Au uwepo wa wajumbe hawa una maslahi kwa namna moja au nyingine kwa mheshimiwa sana?
No comments:
Post a Comment