TUNDA
la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara
10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti
umebaini.
Utafiti
huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, umeeleza
kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na
mfadhaiko.
“Maajabu
ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo
kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo
au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza
katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani, mwaka 2010.
Taasisi
ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya
utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika
utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina uwezo wa
kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa kwa umma kwa hofu
ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa
kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia jina la kibiashara la
‘Triamazon’ na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na
Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.
Utafiti
mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa
katika jarida la Bidhaa Asilia ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa
kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti
wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga seli za
saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya mionzi
ifanyavyo.
Tunda
la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho ndicho
chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani. Imeelezwa
kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti,
kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja
na kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia huweza
kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya mfumo wa
fahamu na sukari.
Utafiti
huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo
kinaweza kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa
na madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na kunyonyoka
nywele.
Aidha
huweza kuupa mwili kinga na kukupa nguvu bila madhara yasababishwayo na
dawa nyingine. Tangu mwaka 1976, tunda hilo liliendelea kufanyiwa utafiti katika maabara
binafsi zaidi ya 20duniani.
Stafeli nini?
Stafeli
ni tunda la chanikiwiti ambalo linastawi zaidi katika ukanda wa kitropiki. Mti
wa tunda hilo ni mfupi wa wastani, Wabrazili wanauita Graviola na Waingereza
wanaliita Soursop. Hapa Tanzani stafeli linajulikana kwa jina jingine la
topetope.
“Tuna
kitengo cha masuala ya tiba na mambo mengine lakini hatujawahi kufanyia utafiti
tunda la stafeli wala dawa nyingine yoyote ya saratani,” alisema Dk Massaga
Mtaalamu
wa masuala ya tiba za vyakula, Boniphas Sosthenes wa kituo cha Tiba cha Neema,
jijini Dar es Salaam, alisema anafahamu uwezo huo wa stafeli kutibu saratani,
lakini hajathibitisha kitalaamu.
Daktari
aliyewahi kumtibu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Dk Keisy Mtambo alisema
taarifa za kuwa stafeli linaweza kutibu saratani anazisikia, lakini hana
uhakika “Nasema
sina hakika kwa sababu satani ina hatua mbalimbali na kwa watu tofauti,” alisema.
Alisema
kwa anavyoifahamu saratani, ni vigumu mno kutibika kwa tunda tu, labda kama
tunda hilo limefanyiwa kazi za kitabibu zaidi. “Kuna
saratani kwa watoto, wazee na watu wenye VVU, zina utofauti mkubwa na utafiti
huo haujaeleza bayana,” anasema
No comments:
Post a Comment