Rais Kenyatta. |
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya
Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya baraza lake la
mawaziri lenye wajumbe 18, mwezi mmoja tangu mchakato wa uteuzi kuanza.
Meneja wa hoteli ya Utalii Joseph Ole
Lenku ameteuliwa kwa nafasi ya mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya
kitaifa, na mbunge wa zamani Samuel Kazungu Kambi kuwa waziri wa kazi, usalama
wa jamii na huduma.
"Hatimaye nimeshapeleka majina
bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa," Kenyatta alisema, kwa mujibu wa
gazeti la Daily Nation la Kenya.
Kamati ya bunge ya uteuzi itawachunguza
wawili hao na kupeleka ripoti kwa Bunge la Taifa.
Uteuzi wa Lenku na Kambi unakuja wiki
moja baada ya bunge kupitisha wajumbe wa baraza la mawaziri waliobakia na
kuwaapisha kwa ajili ya nafasi zao.
No comments:
Post a Comment