To Chat with me click here

Friday, May 31, 2013

CHADEMA YAAHIDI KUJENGA ZAHANATI TINGENI



MRATIBU wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ametoa ahadi ya kujenga zahanati ya kata ya Tingeni katika jimbo la Muheza.

Bahweje alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Tingeni, Omary Kanyau, uliofanyika kijiji cha Ukoka.

Alisema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa huduma za afya kwani zilizopo ziko mbali na kwamba chama hicho kina mipango endelevu na wananchi hao.

Akizungamza kwa niaba ya wakazi wanaoishi katika kata hiyo, Shaban Salim, alisema kwa muda mrefu wanateseka bila kupata huduma za afya, hivyo kuwalazimu kwenda kutibiwa katika hospitali teule ilioko wilayani Muheza.

Salim alisema katika kata hiyo mbali na huduma za afya kuna tatizo la daraja ambapo likijaa maji huwezi kuvuka kwenda upande wa pili kitendo kinachopelekea watoto wanaosoma shule katika maeneo hayo kushidwa kuhudhuria masomo kutokana na daraja hilo kujaa maji.

MAREKEBISHO YA HOTUBA YA UPINZANI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE



Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha CUF....na kuishia na maneno…Israel Liberal ‘ sasa isomeke:

“Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International). Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal International Mwaka 1997.

Mwaka huo huo Liberal International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini Uingereza.

Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the rules of equality to sexual minorities and the recognition that homesexuality and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”. Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.

Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org)  kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja. Kupitia umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………”

Ezekiah Dibogo Wenje
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 30 Mei 2013

Thursday, May 30, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA AWAMU YA PILI YATOKA!


Ili kujua matokeo yako mapya bofya hapa:........

Link 1: Matoke CSEE 1

Link 2: Matokeo CSEE 2

Link 3: MAtokeo CSEE 3

Link 4: Matokeo CSEE 4

ZITTO WRITE TO CAMEROON!



The Rt Hon David Cameron, MP,

Prime Minister

27th May, 2013

Dear Prime Minister

Tanzania has had a long and productive relationship with the UK as a development partner. Tanzania is one of the top recipients of aid from UK mainly through DFID on the African continent. In recent years, the UK has helped Tanzania to establish and lay foundations for an accountable and transparent government. Your country’s support to the Tanzanian parliament, our public institutions and civil society organisations has been critical in these efforts.

This support is, however, dwarfed when the amount that Tanzania loses every year to tax evasion and aggressive tax avoidance in taken into account. To large extent, these tax evasions and avoidance are done by Multinational corporations, most of them registered in the United Kingdom. This is a constant challenge for our country – a challenge that undermines the same foundations of accountability that we are striving to strengthen and uphold.

A recent study produced by Global Financial Integrity (GFI) puts estimates of illicit financial flows out of all developing countries at between $858 billion and $1.06 trillion a year. To each 1 USD into Africa as development Aid, 10 USD leave Africa illicitly. Experts argue that Africa is a net creditor to the world as there is more Africa’s money stashed in Offshore than total Africa’s foreign debt. The world must not allow this to continue. We must stop this by crushing these secrecy jurisdictions.

Every year my country Tanzania loses USD 560 million to tax evasion and avoidance. This is the amount that could otherwise have been used to improve Tanzania’s infrastructure, to improve education and health services across the country, which would have translated into and guarantee a better standard of living for majority of citizens of this country. This amount of money of potential tax revenues would have supported the growth of Tanzania’s economy and contribute to the growth of future tax revenues. Between year 2002 and 2008 Tanzania lost around USD 2 Billion through illicit money transfer including Tax evasion, tax avoidance and corruption. The loss is around 5% of Tanzania GDP.

Some of this money is held in British Overseas Territories and Crown Dependencies. Tanzania and other developing countries in Africa have been finding it hard to tame this trend because of financial secrecy laws.

Strong action by your government can stop this financial secrecy as maintaining those amounts to abusing developing countries and its supporter’s struggles. Quashing such secrecy jurisdictions would have real impact on the lives of many poor Tanzanians, in particular and Africans in general.

In my district of Kigoma, western Tanzania, maternal mortality rate is 933 out of every 100,000 live births. This trend is largely contributed by poor health services. The Government is incapacitated to provide better health services because of low revenue base. Tax havens and secrecy jurisdiction is one of the fundamental reason for this low revenue base.

I sincerely believe that a decision by the G8 to enforce transparency laws and regulations in regards to offshore tax havens is pivotal to supporting our endeavours as a country to do the same. With 5% of GDP lost every year to tax evasion and tax avoidance, Tanzania can no longer afford to ignore this obstacle to our growth and development struggles. Neither can our development partners.

I take this opportunity to commend your leadership in fighting tax evasion and aggressive tax avoidance and on your decision to make it a priority for the 39th G8 summit at Lough Erne, Northern Ireland in June.

I call on you to demonstrate your leadership at the summit by putting in place aggressive sanctions against British Overseas Territories and Crown Dependencies which continue to provide cover for the siphoning of billions of dollars of our tax revenue. I urge for a mandatory disclosure of details of accounts held in known tax havens. When a government has reasonable grounds to suspect that money held in certain jurisdictions is the proceeds of corruption, tax avoidance or other crimes by its citizens, disclosure should be mandatory in order to enable it recover the diverted funds.

Yours sincerely,


Zitto Kabwe, MP

Tuesday, May 28, 2013

BREAKING NEWS: MSANII WA BONGO FLEVA AFARIKI DUNIA



Johannesburg, Afrika Kausini

                              Albert Mangwea enzi za Uhai wake R.I.P
TASNIA ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania (Bongo Fleva) imepata pigo baada ya msanii mahiri wa Hip Hop Albert Mangwea kufariki Dunia nchini Afrika Kusini.

Taarifa iliyonaswa na Vyanzo vyetu vya habari kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba msanii huyo amefariki leo. "Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To The P. ilipofika asubuhi ya leo hawakuweza kuamka mapema kama ilivyo kawaida yao na tulipokwenda kuwagongea tukakuta mlango wao uko wazi tuliingia ndani lakini hakuweza kuamka"alisema shuhuda wa tukio hilo.

Akizungumza na Vyanzo vyetu vya habari kwa nija ya simu akiwa nchini Afrika ya Kusini shuhuda wa tukio hilo alisema kwamba walipojaribu kuwatingisha hali haikuwa ya kawaida huku Mangwea akiwa ameshafariki Dunia na mwenzake M To The P akiwa hoi kiasi cha kupoteza fahamu.

Vyanzo vyetu vya habari ilimtafuta Hussein Oroginal aliyepo Pretoria ambaye alieleza kwamba hata yeye amepata taarifa za kifo cha Mangwea na tayari uchunguzi wa awali wa Madaktari umebaini kwamba wasanii hao walikuwa wamekunywa pombe nyingi kupita kiasi usiku wa kuamkia leo lakini haijajulikana kwamba pombe walizokunywa ni za aina gani.

"Nikweli Mangwea amefariki Dunia na tayari Madaktari wa Hospitali ya  St Hellena Joseph, ilipohifadhia mwili wa marehemu wanasema kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba. marehemu alikuwa amekunywa Pombe nyingi kupita kiasi, ingawa hawajaweza kusema kwamba pombe alizokunywa zilikuwa za aina gani," alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Marehemu Mangwea akiwa jijini Dar es Salaam, huku akiomba jina lake lisiandikwe mtandaoni kwakuwa yeye si msemaji wa familia.