Habari
zilizotufikia katika mtandao wetu ni kuwa, aliyekuwa kiongozi na mwanzilishi wa
kundi la vijana ambao wamekuwa wakijiita “MBWA MWITU” ambaye anafahamika kwa
jina la bandia kama KASELA amekamatwa jana majira ya saa 7 mchana, maeneo ya
Yombo Buza, ambako alikutwa akicheza POOL TABLE.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema kuwa, Kasela alikutwa akicheza pool table na baadhi ya
raia wema, ndipo walipoamua kuwataarifu polisi juu ya uwepo wake eneo hilo.
Polisi hawakuchukua muda wakawa wamefika eneo la tukio kabla mshukiwa
hajastukia mpango huo. Baada ya kijana huyo kuwatambua askari polisi, alitimua
mbio ambazo hazikufua dafu kwa askari hao ambao walikuwa na bunduki zao mkononi
pamoja na baadhi ya raia wema waliojitolea kusaidia polisi. Polisi walifanikia
kumnasa Kasela baada ya kujisalimisha kwao, alipoamrishwa kusimama.
Yasemekana
kijana huyu alizaliwa tarehe 28 December 1995 na anaishi na wazazi wake wote
wawili (Baba na Mama) ambao nao walikwisha onja joto ya jiwe ya motto wao,
baada ya kuwachapa makonde kwa kuwa walimsema katika kumrekebisha tabia.
Mbali
na kuwa yeye ndiye muasisi wa kundi hilo la vijana wadogo wa mbwa mwitu, kijana
huyo amekwisha shiriki katika matukio mbalimbali ya wizi na umwagaji damu katika
maeneo ya Yombo Vituka Lumo, Kiwalani na Buza. Matukio hayo ndiyo yaliyopelekea
wananchi wa maeneo tajwa kujawa na hasira kiasi cha kuwasaka mbwa mwitu hao na
kupelekea vifo vya wanakundi hilo wawili waliotambulika kwa majina ya Mpolendi na
Traveller, huku wengine wakikimbilia mikoa ya jirani kama vile Tanga na
Pwani.
Kwa
sasa hali ni swali katika maeneo hayo, na wananchi wamepokea kwa furaha sana
taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la mbwa mwitu.
Mwisho
kabisa kwa niaba yangu binafsi pamoja na wadau wengine wote wa blog yetu,
napenda sana kulipongeza jeshi la polisi, kwa kuweza kufanikisha kumkamata
kijana huyo ambaye amekuwa tishio na gumzo kwa wakazi wa maeneo taja. Ni
matumaini yangu kuwa sharia itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment