To Chat with me click here
Showing posts with label Bunge. Show all posts
Showing posts with label Bunge. Show all posts
Wednesday, March 19, 2014
Friday, May 31, 2013
MAREKEBISHO YA HOTUBA YA UPINZANI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE
Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya
pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa
upande wa chama cha CUF....na kuishia na maneno…Israel Liberal ‘ sasa
isomeke:
“Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali
chama hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International).
Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal
International Mwaka 1997.
Mwaka huo huo Liberal International
ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya
Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika
tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini
Uingereza.
Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja
wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the
rules of equality to sexual minorities and the recognition that homesexuality
and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”. Kwa
Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya
21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na
usagaji kama matendo halali.
Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja
huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa
Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha
Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org)
kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu
mmoja mmoja. Kupitia umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC
ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel
Liberal………”
Ezekiah Dibogo Wenje
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa
30
Mei 2013
Monday, May 20, 2013
SUGU AUNGURUMA: BUNGE LAAHIRISHWA MPAKA JIONI!
Hutuba ya Sugu bungeni yasimamishwa, Bunge laahirishwa ghafula mpaka jioni, kamati ya uongozi yakutana kuijadiri ni baada ya Zambi kuomba muongozo akidai hotuba ya sugu imejaa uchochezi na uongo wa kuisema vibaya serikali ya ccm.
HII NDIYO HOTUBA
ILIYOSOMWA NA SUGU TOKA KAMBI YA UPINZANI
MSEMAJI MKUU
WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA
WA FEDHA 2013/2014
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’
Mheshimiwa Spika,
Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!
2. UHURU WA UHARIRI NA USALAMA WA WANAHABARI
Mheshimiwa Spika,
Kwa masikitiko makubwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalitaarifu Bunge lako tukufu kwamba sasa Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya fedheha (The List of Shame) ya mataifa ambayo taaluma ya habari ni taaluma ya hatari kwa wale wote wanaoitumia kama sehemu ya wajibu wao kwa taifa na kama ajira yao. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari Ulimwenguni (the Committee to Protect Journalists - CPJ) iliyotolewa mwaka huu 2013, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPJ mwaka 1992, Tanzania imeingizwa kwenye orodha ya nchi 20 ambazo ni hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kutokana na hatari ya kuuwawa kwa mwaka 2012 (20 Deadliest Countries in 2012). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilishikilia nafasi ya 7 ulimwenguni kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa kuhatarisha maisha ya waandishi wa habari.
Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa taarifa ya CPJ, tishio kubwa kwa waandishi wa habari duniani ni kuuwawa kwa kutekwa na kuteswa na/au kutishiwa maisha. Aidha, Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ni washiriki wakubwa wa mauaji ya waandishi wa habari. Kwa mujibu wa takwimu za CPJ, kati ya waandishi waliouwawa mwaka 2012, karibu ya 20% waliuwawa ama na maafisa wa serikali au na majeshi yake. Karibu idadi hiyo hiyo ya waandishi wa habari waliuawa kwa sababu ya kufuatilia taarifa za kiuchunguzi na za hatari. Taarifa hiyo inaonyesha kwamba hadi kufikia Aprili 2013, waandishi wa habari wapatao 30 tayari wamekwishauawa ulimwenguni wakati wakitimiza wajibu wao; wakati mwaka 2012 waandishi wa habari 103 waliuwawa ulimwenguni kote.
Mheshimiwa Spika,
Taarifa ya CPJ inaungwa mkono na ushahidi wa matukio mengi yanayodhihirisha kwamba maisha ya waandishi wa habari wa Tanzania yako hatarini kutokana na vitendo na vitisho kutoka kwa Serikali na watendaji wake ambao hawataki kusikia ukweli dhidi yao ukianikwa hadharani. Kudhihirisha kauli hii tunaomba kumnukuu mwanahabari mahiri na mmoja wa wahanga wa vita dhidi ya wanahabari na uhuru wa habari hapa nchini, Mzee Ndimara Tegambwage:
“Mwaka 2006, waliojiita wananchi wakazi wa jiji la Mwanza, walikusanywa na wenye uwezo kufanya maandamano makubwa kwa walichoita ‘kupinga mwandishi Richard Mgamba kuandika uongo’ na kudai kwamba alikuwa Mkenya na ‘siyo raia wa Tanzania.’ Desemba 2009, mwandishi Frederick Katulanda wa Mwanza, alivamiwa nyumbani. Wavamizi walikuwa wakipaza sauti na kudai kuwa ana nyaraka za akaunti za benki za Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Walikuwa na mapanga. Walikuwa wakichagizana kwa kusema, “Kata kichwa! Kata kichwa!” Waliondoka na mafaili. Walimwachia kilema mguuni na makovu mikononi.
“Mwezi Septemba, 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, katika eneo la Nyambiti, Jimbo la Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, mwandishi Frederick Katulanda alivamiwa na kupigwa na watu wapatao 15 waliojiita “Green Guard” - wa “chama cha kijani.” Katika “kumshughulikia,” Katulanda anasema, walikuwa wakionyesha kuwa na ujuzi mkubwa wa judo na karate huku wakidai kuwa anawaandika ‘vibaya’ Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Mwaka 2011 mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa katika eneo la Igoma, jijini Mwanza. Vyombo vya habari viliripoti kuwa macho yake yalikuwa yametobolewa na kuwekwa gundi aina ya super glue; mguu wa kushoto na mbavu vilikuwa vimevunjika. Vyombo vya habari viliripoti kuwa Massatu aliyekuwa mmiliki na mhariri mkuu wa gazeti la Kasi Mpya (sauti ya umma), alionekana mara ya mwisho usiku wa kifo chake akiwa na maofisa wa polisi na usalama katika baa iitwayo Cross Park katika eneo la Igoma.
“Tarehe 3 Januari, maiti ya mwandishi Issa Ngumba iliokotwa katika pori la mlima Kajuruheta, kijiji cha Mhange, wilayani Kakonko katika mkoa wa Kigoma.Ngumba alikuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizela. Tangu mwezi uliopita Machi, mwandishi wa habari Erick Kabendera anayeishi Dar es Salaam, anaishi kwa wasiwasi. Wazazi wake waishio Bukoba, wamehojiwa na ‘ofisa usalama’ kwa kile kilichoitwa ‘uhalali wa uraia wao.’
“Kuuwawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV, John Lubungo ambaye alikuwa mfuatiliaji mahiri wa habari zinazohusu wafanyabiashara au biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo inadaiwa kufanywa na watu wakubwa nchini, wakiwemo vigogo serikalini. Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliotishwa na wanaoendelea kutishwa; waliopigwa na polisi na askari magereza (Ukonga, Dar es Salaama) kwa tuhuma mbalimbali; waliotishiwa maisha kwa simu na hata kwa kufuatiliwa na watu wasiowafahamu.”
Kwa sababu ya uadilifu na kutopenda kujikweza, Mzee Tegambwage hakutaja shambulio la tindikali na mapanga dhidi yake na mwandishi mwenzake Saed Kubenea wa gazeti la Mwanahalisi, ambalo baadae lilifungiwa na Serikali hii ya CCM.
Saturday, May 18, 2013
ZITTO, MNYIKA WAPASUA BUNGE
![]() |
| Mhe. Zitto Kabwe |
WABUNGE wa CHADEMA; Zitto Kabwe (Kigoma
Kaskazini) na John Mnyika (Ubungo), wamewachochea wabunge wenzao wasihudhurie
semina iliyoandaliwa leo na Wizara ya Nishati na Madini. Sababu waliyoitoa
wabunge hao juu ya ushawishi huo ni kuwa serikali imeanza ugawaji wa vitalu
vipya vya mafuta na gesi kwenye bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.
Hata hivyo, hatua hiyo imeonekana
kuwagawa wabunge, ambapo baadhi wamepinga na wengine kuunga mkono. Kupitia
taarifa zao kwa vyombo vya habari walizozituma kwa nyakati tofauti, Zitto na
Mnyika wamepinga uamuzi wa serikali wa kuanza mzunguko wa nne wa ugawaji wa
leseni za utafutaji na ugunduzi wa gesi nchini.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari, Zitto ameonesha kushangazwa na uamuzi huo wa serikali, kwani Tanzania
bado haijawa na sera ya gesi asilia na kwamba ndiyo kwanza wabunge wamepewa
rasimu ya sera hiyo kwa ajili ya kutoa maoni yao.
“Kesho Jumamosi wabunge tumealikwa
kwenye semina kuhusu sera ya gesi asilia. Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena
zipo kwenye lugha ya kimombo,” alisema Zitto na kuongeza; “Jambo la kushangaza
ni kwamba wakati sera ya gesi asilia ipo kwenye rasimu na ndiyo kwanza wabunge
tumeletewa kutoa maoni, serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya
mafuta na gesi kwenye bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.”
![]() |
| Mhe. John Mnyika |
Pia katika taarifa hiyo Zitto ameelezea
kushangazwa na hatua hiyo ya serikali ambayo alisema inakwenda kinyume cha
maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayozuia ugawaji mpya wa
vitalu hadi sera ya gesi asilia na sheria ya gesi vikamilike.
“Haraka hii ya serikali kugawa vitalu
bila sera wala sheria inatoka wapi? Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho
za semina hii na kuhalalisha maamuzi yasiyozingatia maslahi ya taifa kwa vizazi
vya sasa na vijavyo,” alisisitiza Zitto.
Zitto amewataka wabunge na wananchi
kuupinga uamuzi huo wa serikali.
“Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila
kwanza kuwepo kwa sera na sheria mpya unapaswa kupingwa kwa nguvu zote. Tafuta
mbunge wako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali. Tumalize kwanza sera
na sheria ndiyo tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi,” imesisitiza
taarifa hiyo.
Thursday, February 7, 2013
HALIMA MDEE ATIMULIWA
| Mbunge wa Kawe Chadema - Halima Mdee |
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee,
ametimuliwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge, kwa madai kwamba ana maslahi ya upande mmoja katika mgogoro
uliotokea bungeni juzi wakati Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe,
alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Taarifa za uhakika zilizopatikana bungeni jana zilieleza kwamba Mdee ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, alizuiwa kuhudhuria kikao kilichojadili sakata hilo kwa kuwa alikuwa akishabikia vurugu bungeni.
Taarifa zaidi zimedai kwamba kumeibuka mvutano kuhusu kanuni iliyotumika kumruhusu Waziri Maghembe kutumia nusu saa kujibu hoja ya Mnyika wakati alipaswa kutumia dakika 15 kama wachangiaji wengine.
Jana Mdee alithibitisha kuwa alizuiwa kuhudhuria kikao cha kamati hiyo kwa maelezo kuwa ana maslahi na upande wa kambi ya upinzani juu ya suala la mgogoro wa hoja ya Mnyika ambayo ilipokwa na serikali juzi na kuiua.
Mdee alielezwa kuwa alikuwa bungeni siku hiyo na alishiriki katika kadhia iliyosababisha Bunge kuahirishwa kabla ya muda wake baada ya wabunge wote wa Chadema na NCCR-Mageuzi kusimama kwa muda mrefu na kuzuia shughuli za Bunge kuelendelea wakipinga kitendo cha kuvunjwa kwa kanuni za Bunge kwa kuipa nafasi serikali uondoa hoja binafsi ya Mnyika juu ya upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam.
Kamati ya Maadili imepewa jukumu la kuchunguza chanzo cha vurugu hizo kwa kuwahoji wabunge waliohusika na kadhia ya Jumatatu jioni ili kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa dhidi yao.
WAJUMBE WA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi (Mwenyekiti); Christopher Ole Sendeka; Rashid Ali Abdallah, Dk. Maua Daftari; John Chiligati; Dk. Christina Ishengoma; Riziki Omar Juma; David Kafulila; Vita Kawawa; Philemon Ndesamburo; Augustino Masele, Said Arfi; Augustine Mrema; Cynthia Ngoye; Halima Mdee na Gosbert Blandes.
Hata hivyo, Chadema imewaelekeza wabunge wake wote kutoitikia wito wa kamati hiyo hadi hapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, atakapotoa uamuzi wa rufaa 10 ambazo wabunge hao wamekata kwake, lakini amezikalia tangu mwaka 2011.
Pia Chadema kimetishia kuwasilisha hoja ya kumng'oa madarakani Spika Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai, kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge kwa kutotenda haki kwa pande zote, hasa kambi ya upinzani, kwa maana hiyo wamepoteza sifa za kuongoza muhimili huo.
WABUNGE HAWAJAHOJIWA
Wakati huo huo, Kamati hiyo bado haijawahoji wabunge wanaodaiwa kufanya fujo ndani ya Bunge.
Katika hatua nyingine, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, amesema kitendo cha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtuhumu kuwa ni mropokaji namba moja bungeni ni kwa sababu ya chuki na upendeleo dhidi ya wabunge wa upinzani.
Lissu jana alisema siyo kweli kwamba amekuwa ni mropokaji bungeni kama Spika Makinda alivyomtuhumu na kwamba amekuwa akifuata kanuni zinazotakiwa kwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuisimamia na kuishauri serikali.
Alisema yeye ni miongoni mwa wabunge wachache ambao wanazifahamu kanuni za Bunge, Katiba ya nchi na sheria mbalimbali.
“Kuniita mropokaji ni kunifananisha na baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawajui sheria wala wajibu wa Bunge…wanadhani kazi ya mbunge ni kuikingia kifua serikali na kuitetea, wamesahau kwamba wajibu wao ni kuishauri na kusimamia, " alisema.
Lissu alisema kamwe hawezi kuogopa kuisimamia serikali kama Katiba inavyomtaka na hawezi kuitetea pale inaposhindwa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Taarifa za uhakika zilizopatikana bungeni jana zilieleza kwamba Mdee ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, alizuiwa kuhudhuria kikao kilichojadili sakata hilo kwa kuwa alikuwa akishabikia vurugu bungeni.
Taarifa zaidi zimedai kwamba kumeibuka mvutano kuhusu kanuni iliyotumika kumruhusu Waziri Maghembe kutumia nusu saa kujibu hoja ya Mnyika wakati alipaswa kutumia dakika 15 kama wachangiaji wengine.
Jana Mdee alithibitisha kuwa alizuiwa kuhudhuria kikao cha kamati hiyo kwa maelezo kuwa ana maslahi na upande wa kambi ya upinzani juu ya suala la mgogoro wa hoja ya Mnyika ambayo ilipokwa na serikali juzi na kuiua.
Mdee alielezwa kuwa alikuwa bungeni siku hiyo na alishiriki katika kadhia iliyosababisha Bunge kuahirishwa kabla ya muda wake baada ya wabunge wote wa Chadema na NCCR-Mageuzi kusimama kwa muda mrefu na kuzuia shughuli za Bunge kuelendelea wakipinga kitendo cha kuvunjwa kwa kanuni za Bunge kwa kuipa nafasi serikali uondoa hoja binafsi ya Mnyika juu ya upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam.
Kamati ya Maadili imepewa jukumu la kuchunguza chanzo cha vurugu hizo kwa kuwahoji wabunge waliohusika na kadhia ya Jumatatu jioni ili kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa dhidi yao.
WAJUMBE WA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi (Mwenyekiti); Christopher Ole Sendeka; Rashid Ali Abdallah, Dk. Maua Daftari; John Chiligati; Dk. Christina Ishengoma; Riziki Omar Juma; David Kafulila; Vita Kawawa; Philemon Ndesamburo; Augustino Masele, Said Arfi; Augustine Mrema; Cynthia Ngoye; Halima Mdee na Gosbert Blandes.
Hata hivyo, Chadema imewaelekeza wabunge wake wote kutoitikia wito wa kamati hiyo hadi hapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, atakapotoa uamuzi wa rufaa 10 ambazo wabunge hao wamekata kwake, lakini amezikalia tangu mwaka 2011.
Pia Chadema kimetishia kuwasilisha hoja ya kumng'oa madarakani Spika Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai, kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge kwa kutotenda haki kwa pande zote, hasa kambi ya upinzani, kwa maana hiyo wamepoteza sifa za kuongoza muhimili huo.
WABUNGE HAWAJAHOJIWA
Wakati huo huo, Kamati hiyo bado haijawahoji wabunge wanaodaiwa kufanya fujo ndani ya Bunge.
Katika hatua nyingine, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, amesema kitendo cha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtuhumu kuwa ni mropokaji namba moja bungeni ni kwa sababu ya chuki na upendeleo dhidi ya wabunge wa upinzani.
Lissu jana alisema siyo kweli kwamba amekuwa ni mropokaji bungeni kama Spika Makinda alivyomtuhumu na kwamba amekuwa akifuata kanuni zinazotakiwa kwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuisimamia na kuishauri serikali.
Alisema yeye ni miongoni mwa wabunge wachache ambao wanazifahamu kanuni za Bunge, Katiba ya nchi na sheria mbalimbali.
“Kuniita mropokaji ni kunifananisha na baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawajui sheria wala wajibu wa Bunge…wanadhani kazi ya mbunge ni kuikingia kifua serikali na kuitetea, wamesahau kwamba wajibu wao ni kuishauri na kusimamia, " alisema.
Lissu alisema kamwe hawezi kuogopa kuisimamia serikali kama Katiba inavyomtaka na hawezi kuitetea pale inaposhindwa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Friday, February 1, 2013
SAKATA LA GESI MTWARA: MBOWE AMBANA PINDA
KIONGOZI
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amembana Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, akitaka serikali iwachukulie hatua watendaji waliozembea
kudhibiti vurugu za mzozo wa gesi Mtwara.
Mbowe
pia alimhenyesha Pinda akimtaka alihakikishie Bunge ni lini serikali itakuwa
tayari kuweka wazi mikataba kadhaa ikiwamo ya mafuta na gesi asili ili kuondoa
upotoshaji wa miradi hiyo kama ilivyotokea Mtwara.
Akiuliza
swali hilo bungeni jana mjini hapa, Mbowe alisema kwa kuwa vurugu hizo
zimetokana na uzembe wa kisiasa na viongozi wakiwamo wa vyombo vya dola
kushindwa kubaini na kudhibiti ghasia hizo mapema, kwanini wasichukuliwe hatua
kwa uzembe huo.
Akijibu
maswali hayo, Pinda alirejea kauli yake ya mara kwa mara tangu alipotoka
kusuluhisha mzozo huo Mtwara, akisema vyama vya siasa vimechangia sana kukuza
na kupotosha ukweli wa mradi huo.
Alisema
wanasiasa walitumia mzozo huo kujiimarisha kisiasa na kujijenga kwa ajili ya
uchaguzi unaokuja. "Suala
la kuwawajibisha watendaji hao liko chini ya waziri mkuu na rais,
tutaliangalia,” alisema Pinda.
Hata
hivyo, Pinda alisema jambo la msingi si kutafuta mchawi, kwani tatizo la Mtwara
ni la wote, na siku zijazo kutakuwa na ushirikishwaji wa jamii katika kutoa elimu
ili kuepuka madhara kama yaliyotokea Mtwara.
Kuhusu
kuweka wazi mikataba ili kuondoa upotoshaji, Pinda alisema mikataba hiyo haina
siri na inaweza kuwekwa wazi kupitia mifumo ya kibunge.
Hata
hivyo, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), hakuridhika na majibu hayo na katika maswali yake ya nyongeza
alimtaka waziri mkuu kutamka wazi bila kumng’unya maneno kama serikali iko
tayari kuweka mikataba hiyo wazi.
Pia
alihoji ni kwa nini serikali iko tayari kutekeleza kero za wananchi pale
inapobanwa kwa presha na maandamano kama ilivyotokea Mtwara.
Katika
hoja hiyo, Pinda alisema serikali haiko tayari kuweka wazi mikataba hiyo
kupitia magazeti, kwani mingine ina taratibu zake lakini iko tayari kuweka wazi
kupitia mifumo ya kibunge.
Kuhusu
serikali kusikiliza kero za wananchi baada ya presha za maandamano, Pinda
alisema maandamano si njia sahihi ya kuwasilisha madai ya wananchi. "Ndugu
yangu Mbowe anajaribu kuleta hoja ambayo haina mashiko. Mimi siamini kuwa
maandamano ndiyo njia sahihi ya kuwasilisha malalamiko ya wananchi,” alisema
Pinda.
Mapema
kabla ya maswali kwake, Pinda alitoa taarifa ya kueleza kuhusu vurugu za Mtwara
pamoja na madhara yaliyojitokeza, ambapo hata hivyo alirudia kile alichowaeleza
waandishi wa habari juzi.
Alisema
kulikuwa na upotoshaji mkubwa kwamba bomba hilo la gesi lingeishia Bagamoyo
ambako inajengwa bandari ya kusafirishia gesi hiyo nje na kumhusisha Rais
Jakaya Kikwete, jambo ambalo si la kweli kabisa.
Waziri
Mkuu Pinda aliwatangazia wabunge uharibifu wa mali na hasara iliyopatikana
kutokana na vurugu hizo, sambamba na kuorodhesha majina ya watu waliochomewa
nyumba, magari na mali nyingine.
Pia
alitaja majengo na ofisi za serikali zilizochomwa moto pamoja na magari, ambapo
uharibifu huo umesababisha hasara ya mabilioni ya fedha, akisema serikali
itaangalia namna ya kuwafidia.
Thursday, January 31, 2013
MAKINDA AMPONGEZA LEMA
SPIKA wa Bunge Anna Makinda,
amempongeza Mbunge wa Arusha Mjini, Goodbless Lema (CHADEMA) kwa kurejea bungeni.
Spika alitoa pongezi hizo jana ndani ya
Ukumbi wa Bunge baada ya kumuona mbunge huyo akiingia ukumbini na kuketi kwenye
kiti chake.
“Naona Mheshimiwa Lema anaingia.
Nachukua nafasi kukupongeza kwa kurudi bungeni. Karibu sana,” alisema spika
huku wabunge wengine wakishangilia kwa kupiga makofi.
Lema, mmoja wa wabunge machachari wa
CHADEMA, alikuwa nje ya Bunge kwa takribani miezi kumi baada ya Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha kumvua ubunge.
Kesi dhidi yake ilifunguliwa na
wanachama sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao pamoja na mambo mengine
walidai Lema alimkashifu mgombea wao, DkBatilda Burian.
Hata hivyo, Lema alikata rufaa na
kurejeshewa ubunge wake Desemba mwaka jana.
Tayari Lema ameahidi kufufua hoja zote
alizoziacha bungeni, ikiwemo hoja kwamba Waziri Mkuu alilidanganya Bunge.
Thursday, November 1, 2012
UTORO HUU WA WABUNGE KAMWE HAUKUBALIKI
LICHA ya ukweli
kwamba Bunge ni taasisi iliyo huru na mojawapo ya mihimili mikuu mitatu ya
Dola, kwa Tanzania, mhimili huu kwa siku za karibuni utendaji wake umekuwa
ukitia shaka.
Pamoja na ukweli kwamba Bunge letu linatakiwa kujiendesha kwa uhuru bila kuingiliwa, lakini tukiwa sehemu ya jamii, tunao wajibu wa kulikosoa pale linapokuwa limekwenda kombo na kulipongeza na kulishauri kadri inavyowezekana.
Bunge letu la sasa ambalo linaundwa na vijana wasomi wazuri pamoja na wakongwe wenye uzoefu, linakutana kwa mjini Dodoma tangu juzi. Hata hivyo, lilianza vibaya kwani katika kikao chake cha kwanza cha juzi Jumanne, kililazimika kuahirishwa kulingana na kanuni za kazi zinazosimamia chombo hiki kikuu cha kutunga sheria kutokana na kutotimia akidi ya wabunge wanaotakiwa kupitisha azimio au hata muswada wa sheria, ambao ni nusu ya wabunge wote 357.
Ingawa wabunge wengi wanaweza kujitetea kwa uzembe huo, tayari kitendo hicho ambacho kimetafsiriwa na wengi kama utoro kilisababisha shughuli iliyopangwa siku ile, yaani ya kupitisha Azimio la Bunge la Marekebisho ya Pili ya Ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya, Afrika, Caribean na Pacific (ACP), kukwama.
Hatukufurahishwa na kitendo hiki hasa ikizingatiwa kwamba kimefanyika kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi minne. Mara ya kwanza wabunge kukwamisha shughuli za Bunge ilikuwa wakati wa kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika katika Mkutano wa Nane.
Bajeti hiyo ilikwama wiki moja tu tangu Spika wa Bunge, Anne Makinda kukemea tabia ya utoro akisema ilikuwa imekithiri. Kitendo cha utoro wa mara kwa mara cha wabunge wetu, kikionyesha ama kujisahau, kukosa umakini au wakati mwingine utovu wa nidhamu. Tumekuwa tukieleza mara zote kwamba inafaa kanuni zote zinazosimamia uendeshaji wa chombo hiki zitazamwe upya na ikiwezekana kuwe na hatua zikiwamo za kinidhamu kwa mbunge mmoja mmoja anayekiuka kanuni hizi ikiwamo kutohudhuria mikutano na vikao ipasavyo.
Tunashauri, utaratibu
wa kuwapa ruhusa wabunge kuondoka Dodoma kwa shughuli zao binafsi unafaa nao
uangaliwe upya, kwa umakini, hasa kama ndio unaotoa nafasi kwao kuwa watoro
katika vikao ambavyo gharama zake pia ni kubwa mno. Ni jambo lisilokubalika
kuona kodi za wananchi wa kawaida wa Tanzania, yaani wakulima na wafanyakazi na
kidogo wafanyabiashara ambazo hulipa mishahara au posho nono za wabunge wetu
zinaachwa kutumika vibaya kwa watu ambao hawaoni sababu ya kuhudhuria vikao.
Tunaamini, ofisi ya Spika, Anne Makinda na Katibu wake, Dk Thomas Kashillilah wataliangalia hili upya na uwajibikaji wa kila mbunge ambao baadhi yao wakati mwingine wamekuwa wakipigiwa kelele na wapiga kura wao kwamba wanashindwa kuwawakilisha ipasavyo. Tunashauri Bunge liangalie pia kanuni na kuratibu ziara zote ambazo zimekuwa wakati mwingine zikiruhusiwa kufanywa na wabunge wakati mikutano ya Bunge ikiendelea Dodoma kwani baadhi yao wameondoka huko na kwenda kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Vinginevyo, mienendo ya namna hii ya wabunge wetu kutoonekana bungeni na wananchi kupitia kwenye luninga kuona viti vingi vikiwa tupu, vinatoa picha mbaya si kwao tu, bali taasisi nzima. Wabunge wanapaswa kufahamu kwamba wapiga kura wao wanawafuatilia, baada ya kuwachagua wanategemea kuwaona wakiwajibika ipasavyo bungeni kwa maana ya kuhudhuria vikao na kutoa hoja zenye mustakabali mwema kwa ustawi wao na taifa lao na siyo kufanya shughuli kinyume cha hapo na wanapofika bungeni kuanza kuzomeana na kupigana vijembe.
Tunapendekeza, iwe mwiko kwa mbunge yeyote kuondoka Dodoma hasa wakati wa vikao vya Bunge bila sababu maalumu, na zinazokubalika kama vile za kiafya, kufiwa au zile ambazo haziwezi kutiliwa shaka au kuhojiwa na yeyote. Umefika wakati pia kwa ratiba ya mikutano minne ya Bunge ya kila mwaka kupangwa vizuri ili isiingiliane pasipo sababu za msingi na majukumu mengine ya kitaifa kama vile ziara za viongozi wakuu na mambo mengine kama hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)



