Balozi Khamis Kagasheki |
Dodoma. Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imesema ni
muda mwafaka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
kujiuzulu kutokana na ama kwa kujua, au kutojua kuongoza njama za makusudi
kutaka kumpatia mwekezaji wa Kampuni ya Otterlo Business Corporation (OBC)
katika ardhi ya Loliondo.
Akiwasilisha
maoni ya kambi hiyo kuhusu Makadirio ya Matumizi kwa mwaka 2013/14 ya Wizara ya
Maliasili na Utalii juzi, Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Mchungaji Peter Msigwa
alisema ardhi hiyo wanataka kuitoa kinyume cha sheria.“Huu ni wakati mwafaka
kwa Waziri Kagasheki kuwajibika kwa kujiuzulu kwa hiari yake, au kama
atashindwa kufanya hivyo, kuwajibishwa kwa kufukuzwa kazi kwa kusababisha
mgogoro wa sasa maeneo ya Loliondo na Sale,” alisema.
Alitaka
kujua kama ni kweli kitendo cha hivi karibuni cha Waziri Kagasheki kutoa amri
ya wananchi wa Loliondo na Sale kunyang’anywa maeneo yao mengine na kukabidhiwa
kwa Kampuni ya OBC, kilitokana na maagizo au maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete.
Mchungaji
Msigwa alisema kutokana na Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana kuchunguza mgogoro huo na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM bara,
Mwigulu Nchemba inaonyesha uamuzi huo ulikuwa uamuzi wake.
Hata
hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi
aliilaumu kambi hiyo akisema inatoa kauli ya uongo ili hali ikijua ukweli
kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Nchimbi
alisema mmiliki wa meli ile anaitwa Bus Herman Ledley na walituhumiwa na
kupelekwa mahakamani kwa kosa hilo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Team Fright (T) Ltd, Ladius Tesha, Gabriel Chambo wa Kampuni ya Import and
Export Ltd, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kigoma MN Enterprises Ltd, Shaaban
Yasin Abdullah, mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari ya Dar
es Salaam, Ericleo Morani, mfanyakazi wa Kampuni ya Kigoma MN Enterprises, Issa
Ahmed Rwino na Mawakala wa Kampuni ya T Fright (T) Ltd, Nelbert Kiwale na
Abubakar Omar Hassan.
No comments:
Post a Comment