To Chat with me click here

Wednesday, May 22, 2013

LOWASSA KAMA RAIS ITAKUWA NI KIKWETE 2.0 (MARUDIO YA 2005)




Hawajakutana mtaani; wametoka mbali, na inajulikana kwa wengi kuwa safari yao kuelekea Magogoni ilikuwa na ahadi baina yao kuanzia 1995. Ushirika wao au Ubia wa uongozi wao ulikuwa wazi kuwa yeyote kati yao angeteuliwa kuwa Rais basi mwenzie angekuwa Waziri Mkuu. Matokeo yake Katiba ilifanyiwa mabadiliko 2005 ili kuhakikisha kuwa Waziri Mkuu anakuwa mtu wa tatu kuushika Urais katika Mnyororo wa Kufuatana kiuongozi (Rais, Makamu wa Rais halafu Waziri Mkuu). Kabla yake wa tatu kiuongozi alikuwa ni Spika. Bila ya mabadiliko yale Spika Sitta angekuwa anakaiumu Urais wakati wowote RAis na Makamu hawapo nchini.

Kashfa ya Richmond kama alivyosema Kikwete mbele ya wazee wa Dar ilikuwa ni "ajali ya kisiasa" tu kwa Lowassa. Ilikuwa ni ajali mbaya hata hivyo kwa sababu ilivuruga kwa kiasi kikubwa na imeacha ombwe kubwa sana la kujijenga tena Lowassa. Lakini halikufuta ndoto ya yeye kuutaka Urais; wengine wanaweza kusema ni "haki" yake; aliahidiwa kupokezana; anatoka Kikwete anaingia Lowassa.

Je, utawala wa Lowassa unaweza kuwa tofauti? Well, je nyani akiamua kuondoka shambani na kuwaachia ngedele mahindi yatakuwa salama? Kufikiria kuwa CCM chini ya Lowassa na Tanzania chini ya Lowassa itakuwa tofauti ni kujaribu kukinga mikono jangwani kungojea mvua.

Kwa ufupi, yeyote anayetaka mwendelezo wa utawala wa Kikwete kwa miaka kumi ijayo - ndani ya CCM na kwa taifa - uchaguzi uko wazi - kuhakikisha kuwa Lowassa anachaguliwa kuwa Rais. AU watu watuambie utawala wa Lowassa utakuwa na tofauti gani na utawala wa Kikwete na kwanini?
Lowassa na Jk ni watu wanaofanana kimvuto machoni mwa watu.Kama ni kwa mganga wa kienyeji watakuwa walikwenda kwa mganga mmoja.hata kiutendaji ni watu ambao hawatofautiani sana.Watu wengi walimchaguwa Jk kutokana na mvuto aliokuwa nao kwa watu pia na jinsi alivyo waaminisha watanzania kuwa ndiye mwenye uwezo wa kuwaletea maisha bora watanzania.Maisha bora ambayo yameshindikana kabisa.Lowassa naye pamoja na kuwa na mvuto kwa watu naye anajinasibu kama mtu mwenye kuthubutu mwenye maamzi magumu kauli ambayo imepondwa na Magufuli kuwa anae toa maamzi magumu ni kibaka Rais anatoa maamzi makini.Maneno yote ya kuthubutu na maamzi magumu ambayo lowassa anajaribu kuwaaminisha watz ili wamuone kuwa ndiye mtu pekee ambae anaweza kuwaletea mabadiliko watz lakini hakuna mabadiliko yoyote ambayo anaweza kuyaleta tofauti na Jk.ukizingatia kuwa alikuwa na nafasi kubwa sana serekalini nafasi ambayo angeweza kuitumia kuleta mabadiliko ambayo anajaribu kuwaaminisha watz waamini kuwa anaweza kuwaletea endapo watamfanya kiongozi wao kwa mara nyingine tena.

No comments:

Post a Comment