OFISI
ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis Jorge Mario imepokea
taarifa za Kanisa Katoliki Parokia ya Ollasiti kulipuliwa na bomu nchini
Tanznaia na kuiagiza serikali kutoa taarifa za uchunguzi wa suala hilo haraka.
Taarifa
zilizonaswa na wandishi wetu kutoka vyanzo
vya kuaminika ndani ya kanisa hilo jijini Dar es Salaam zinadai kwamba Papa
Mario ameagiza serikali kutoa taarifa za uchunguzi wa suala hilo haraka.
Papa
Mario amepokea taarifa hizo ambazo zilitangazwa na Rais Jakaya Kikwete kwamba
ni tukio la kigaidi, huku watu watatu wakiuawa na wengine zaidi ya 70
kujeruhiwa katika tukio hilo.
Akizungumza
na Redio Vatican pamoja na mitandao ya kijamii inayomilikiwa na Kanisa hilo
kubwa Duniani, mwakilishi wa Papa huyo Francisco Montecillo Padilla
alisema kwamba tukio hilo halikutarajiwa kabisa kwa sababu muda wote kulikuwa
na hali ya utulivu na amani kanisani hapo.
"Nilipata
mshtuko baada ya kusikia mlipuko wa bomu hilo, na sekunde chache nikaona
majeruhi wengi wamelala chini, nikapatwa na wasi wasi huku nikiwaonea huruma
majeruhi wasiokuwa na hatia lakini Askari Polisi waliwahi kunichukuwa na
kunipeleka sehemu iliyotulia kwa usalama zaidi"alisema
Askofu Montecillo Padilla.
Hata
hivyo taarifa zaidi zinasema kwamba Ofisi ya Papa Francis tayari imeiagiza
Serikali ya Tanzania kuhakikisha inakamilisha uchunguzi wa suala hilo haraka,
huku pia ikionyesha nia ya kutoa msaada zaidi kwa serikali katika uchunguzi
wake. Hata hivyo Ofisi ya Kiongozi huyo tayari imesha agiza Kikosi cha
upelelezi cha kimataifa kutoka nchini Marekani FBI kuja nchini kuongeza nguvu
katika upelelezi wa tukio hilo,tukio la aina hiyo halikuwahi kutokea nchini
Tanzania, ila liliwahi kutokea katika nchi jirani ya Kenya.
No comments:
Post a Comment