MRATIBU wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ametoa ahadi ya kujenga
zahanati ya kata ya Tingeni katika jimbo la Muheza.
Bahweje alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye
mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Tingeni, Omary Kanyau,
uliofanyika kijiji cha Ukoka.
Alisema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa
huduma za afya kwani zilizopo ziko mbali na kwamba chama hicho kina mipango
endelevu na wananchi hao.
Akizungamza kwa niaba ya wakazi wanaoishi katika
kata hiyo, Shaban Salim, alisema kwa muda mrefu wanateseka bila kupata huduma
za afya, hivyo kuwalazimu kwenda kutibiwa katika hospitali teule ilioko
wilayani Muheza.
Salim alisema katika kata hiyo mbali na huduma za
afya kuna tatizo la daraja ambapo likijaa maji huwezi kuvuka kwenda upande wa
pili kitendo kinachopelekea watoto wanaosoma shule katika maeneo hayo kushidwa
kuhudhuria masomo kutokana na daraja hilo kujaa maji.
No comments:
Post a Comment