Rais wa Marekani Barrack Obama ambaye
anatarajiwa kudhuru Tanzania siku za hivi karibuni
Kwa ufupi;
Akizungumza na Mwananchi Jumapili
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa Rais
Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na wataalamu wa
masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa ujio wa
Rais Barack Obama wa Marekani nchini, ni fursa nyingine kwa Tanzania kukuza
uchumi na kuimarisha uwekezaji.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa Rais
Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na wataalamu wa
masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Ziara yake ya kwanza aliifanya wakati
wa awamu yake ya kwanza madarakani, wakati ziara ya safari hii ni kipindi chake
cha lala salama.
Rais Obama alianza rasmi awamu yake ya
kwanza kama Rais wa Taifa kubwa, Januari 20, 2009, wakati ng’we yake ya mwisho
ilianza Januari 21, 2013.
Rais Obama anatarajiwa kufanya ziara
hiyo mwishoni mwa Juni mwaka huu, ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za
mwanzo za Afrika Mashariki kutembelewa na kiongozi huyo.
Ziara ya Rais Obama inafanyika baada ya
ziara ya Rais Xi Jiping wa China aliyeitembelea Tanzania Machi 28, mwaka huu,
ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya kwanza kuitembelea kwa Afrika tangu
achaguliwe kuwa rais, Machi 14, 2013.
Akizungumzia ziara hiyo tarajiwa,
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye
ni mchumi, alisema amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia ya vyama
vingi kwa kulinganisha na nchi nyingine za jirani, vimechangia kuwapo kwa ziara
hiyo.
Profesa Lipumba alisema pia ugunduzi wa
rasilimali za asili kama vile gesi, mafuta na madini ya urani ni sababu
nyingine iliyomfanya Rais huyo kuja nchini. Hivyo aliwashauri viongozi wa Serikali
kujipanga kwa ajili ya kufungua mlango huo mwingine wa uchumi na uwekezaji.
Alisema pamoja na hali hiyo pia kuna
mambo ambayo yanaweza kuchafua taswira ya nchi kama vile ubovu wa miundombinu
ya barabara, msongamano wa magari barabarani na msongamano wa meli bandarini
wakati zikisubiri kushusha mizigo.
Jumatano ya wiki iliyopita, Waziri wa Mambo
ya Nje wa Marekani, John Kerry alitangaza mbele ya wajumbe wa Kamati ya
Ushirikiano kati ya Marekani na Afrika, kwamba Rais Obama hivi karibuni
atafanya ziara Afrika.
Ingawa Kerry hakutoa maelezo zaidi ya
nchi gani za Afrika ambazo Rais Obama atazitembelea, lakini baadhi ya vyombo
vya habari vya Nigeria vilieleza kiongozi huyo atafanya ziara Tanzania, Rwanda
na Nigeria.
Kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana
na Rais Obama tangu awe Rais wa Marekani, alikuwa Rais Jakaya Kikwete
aliyekutana naye Mei 2009, Washington, Marekani.
Kwa nini ni Tanzania na Rwanda
“Kenya asingeweza kwenda kutokana na
suala la Rais na Makamu wake kutuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari
yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu 2007/2008, kwani msimamo wa Marekani ni
kutaka wahusika wa vitendo vile wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Hivyo kwake
kuwatembelea watuhumiwa asingeeleweka,” alisema Profesa Lipumba.
Alibainisha kuwa Rwanda ina uhusiano wa
karibu na Marekani na pengine suala la mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC) litachukua nafasi.
Kulingana na taarifa za Ikulu ya
Marekani, Rais Obama alikuwa amepanga muda wake mwingi wa awamu ya pili ya
uongozi wake kujihusisha na masuala ya Afrika.
No comments:
Post a Comment