 To Chat with me click here
To Chat with me click here
          
        
          
        
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)
Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara
  
 Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
  
 
|  | 
| Mhe. Zitto Kabwe | 
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo 
kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na
 baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata 
hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo 
wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI 
na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania.  Suala la USIRI lipo Wizara  ya 
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.  Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya 
Viwanda na Biashara.
  
 USIRI
 Biashara hii ya “Ring Back 
Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua
 maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao  nao huingia mikataba
 na Wasanii (Content Creators).
 Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa 
nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content
  Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii.  
Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine
 (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ 
nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii.  Wachuuzi (Content 
Providers) nao  hawatoi taarifa za  mauzo kwa wasanii na wanatumia 
uelewa mdogo wa  wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya.  Matokeo 
yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya 
mapato ghafi ya kazi yake.  Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover)
 ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.
  
 Suluhisho:
 
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) 
zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na 
biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure 
rules).  Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila
 kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
  
 UNYONYAJI
 Kutokana na usiri
 ulioelezwa hapo juu, wasanii  wamekuwa wakinyonywa kimapato.  Kwa mfano
 Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake 
(wimbo) katika mwezi (downloads).
  
 Lakini mapato yatokanayo na 
“subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati
 chochote.  Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja 
kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za 
‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44
 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.
  
 Nchini Marekani 
biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public 
Performances)  na hivyo “copyright Association” ya Marekani imeweka 
kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa.  
Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi 
yake kama muito wa simu.
  
 SULUHISHO
 Serikali kupitia Wizara
 ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii 
kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za 
simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya  mapato ghafi, ambapo 
asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya 
usimamizi  na Ulinzi wa kazi za Wasanii.
  
 HITIMISHO
 Kanuni 
za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na 
mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho 
endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali 
kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze 
kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013
  
Kabwe Z. Zitto, (Mb)
 Kigoma Kaskazini
 Dodoma, 13 Mei 2013.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment