MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA)
amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa kutumia kura zao vizuri
katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa kuiondoa madarakani Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi kutokana na kudidimiza uchumi na kutoleta maendeleo nchini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya
kualikwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa CHADEMA walioko mkoani hapa, Lissu alisema
Serikali ya CCM imeshindwa kumkomboa mwananchi kutokana na wabunge na viongozi
wake kutokuwa na uchungu na nchi.
Alisema ni kazi kubwa kwa sasa kwa mwananchi kupata
maendeleo chini ya CCM, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuitumia kura yake
kuwachagua wabunge wengi wa upinzani na upande wa rais.
“Kila Mtanzania anajua kuwa utawala wa CCM ni giza
tupu, angalieni maisha ya walimu, askari, wakulima na wafanyakazi, wako katika
hali ngumu sana,” alisema.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kumsifu Mbunge wa
Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwa kazi anayofanya katika kutetea maslahi
ya taifa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla kutokana na kusimama kidete bungeni.
No comments:
Post a Comment