Idadi
ya tembo wa Tanzania aina ya jumbo inaweza kutokomezwa ndani ya miaka saba
ikiwa ujangili utaendelea katika viwango vya sasa, mwenyekiti wa kamati ya
bunge juu ya ardhi, mazingira na maliasili James Lembeli aliliambia Bunge la
Taifa siku ya Jumanne (tarehe 30 Aprili).
Kwa
mujibu wa Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Tanzania ilikuwa
na tembo 109,000 mwaka 2009, lakini kuwa na kasoro ya tembo ya 70,000 mwaka
2012.
"Ikiwa
mwenendo huu wa ujangili utaachiwa bila ya kushughulikiwa, ni wazi kuwa idadi
ya tembo itapotea ndani ya miaka saba ijayo," Lembeli alisema kwa mujibu
wa gazeti la The Guardian la Tanzania. "Hili ni janga la taifa. Serikali
na mashirika yake inapaswa kuchukua hatua makini ili kushugulikia tatizo
hili."
Lembeli
alitoa wito kwa serikali kuipitia Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009, kutoa
adhabu kali zaidi kwa majangili, kuajiri walinzi zaidi wa mbuga na kutoa vifaa
na silaha za kisasa ili kupambana na ujangili.
Kwa
dhamiri hiyo, aliomba bajeti ya kamati yake ya takriban shilingi bilioni 75.5
(dola milioni 46.5) kwa mwaka wa fedha 2013-2014.
No comments:
Post a Comment