Johannesburg, Afrika Kausini
TASNIA
ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania (Bongo Fleva) imepata pigo baada ya
msanii mahiri wa Hip Hop Albert Mangwea kufariki Dunia nchini Afrika Kusini.
Taarifa
iliyonaswa na Vyanzo
vyetu vya habari kutoka Afrika Kusini zinasema
kwamba msanii huyo amefariki leo. "Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To
The P. ilipofika asubuhi ya leo hawakuweza kuamka mapema kama ilivyo kawaida
yao na tulipokwenda kuwagongea tukakuta mlango wao uko wazi tuliingia ndani
lakini hakuweza kuamka"alisema shuhuda wa tukio hilo.
Akizungumza
na Vyanzo vyetu vya
habari kwa nija ya simu akiwa nchini Afrika ya Kusini shuhuda wa
tukio hilo alisema kwamba walipojaribu kuwatingisha hali haikuwa ya kawaida
huku Mangwea akiwa ameshafariki Dunia na mwenzake M To The P akiwa hoi
kiasi cha kupoteza fahamu.
Vyanzo vyetu vya habari ilimtafuta Hussein
Oroginal aliyepo Pretoria ambaye alieleza kwamba hata yeye amepata taarifa za
kifo cha Mangwea na tayari uchunguzi wa awali wa Madaktari umebaini kwamba
wasanii hao walikuwa wamekunywa pombe nyingi kupita kiasi usiku wa kuamkia leo
lakini haijajulikana kwamba pombe walizokunywa ni za aina gani.
"Nikweli
Mangwea amefariki Dunia na tayari Madaktari wa Hospitali ya St
Hellena Joseph, ilipohifadhia mwili wa marehemu wanasema kwamba uchunguzi wa
awali unaonyesha kwamba. marehemu alikuwa amekunywa Pombe nyingi kupita kiasi,
ingawa hawajaweza kusema kwamba pombe alizokunywa zilikuwa za aina gani,"
alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Marehemu Mangwea akiwa jijini Dar es
Salaam, huku akiomba jina lake lisiandikwe mtandaoni kwakuwa yeye si msemaji wa
familia.
No comments:
Post a Comment