Dodoma,Tanzania
|
WAKATI
Watanzania wakijiandaa kufuatilia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mafunzo
ya Ufundi leo Waziri wa Wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa anatarajia kukutana na
upinzani mkali, kutoka kwa wabunge wa pande zote mbili yaani Upande wa Upinzani
na Wapunge wa CCM.
Habari
zilizonaswa na Vyanzo vyetu vya habari zinadai
kwamba, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya
Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya CCM mjini Dodoma zinadai kwamba, Wabunge hao
wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo ajiuzuru ili
kukisafisha Chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli kwa Wanafunzi
mwaka huu.
"Hotuba
ya Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama Kawambwa hata jiuzuru,
hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika
setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ndiyo
inayochangia kuharibu Chama"kilisema chanzo hicho kwa masharti ya
kutotajwa majina yake na kuongeza:
"Huu
mpango unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshma ya
Chama, lakizima tuanzie ndani kuwajibishana wenywe kabla ya wapinzani kuanza,
kwani tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi na hatimaye
watazidi kuichukia Serikali". Wakati Waziri Dk Kawambwa akiandaliwa
mazingira ya kung'olewa, Necta inatarajia kutangaza matokeo yaliyoongeza kiwango
cha ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57, wiki hii pamoja
na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
No comments:
Post a Comment