Chama
cha upinzani cha Tanzania CHADEMA kimetishia kuandamana mbele ya Wizara ya Maji
kuchochea serikali kuchukua hatua kuhusiana na upungufu mkubwa wa maji jijini
Dar es Salaam, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.
Mbunge
wa Ubungo John Mnyika alitangaza kusudio la chama kupinga wakati wa matembezi
kutoka eneo la Veterinari hadi viwanja vya Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam.
Waandamanaji wamempa Waziri wa Maji Jumanne Maghembe wiki mbili kufafanua mbele
ya umma wizara inafanya nini kushughulikia matatizo ya maji jijini.
Mwaka
jana, utafiti ulionyesha kwamba karibia asilimia 77 ya wakaazi wa Dar es Salaam
hawapati maji ya kutosha. Maghembe aliliambia bunge kwamba serikali imepanga
kuwa na zaidi ya mara mbili ya usambazaji wa maji jijini Dar es Salaam ifikapo
mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment