Mzee Amos Kaguta Museveni (96) |
KAMPALA,
Uganda
“Rais
Museveni na familia yote ya Kaguta, inasikitika kutangaza kifo cha baba yao
mpendwa Mzee Amos Kaguta, 96, ambacho kimetokea leo Februari 22 saa 1 asubuhi
kwenye Hospitali ya Kimataifa ya Kampala”
MZEE
Amos Kaguta Museveni, baba mzazi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda (pichani
kulia), amefariki dunia leo asubuhi, taarifa kutoka Ikulu zimethibitisha kifo
hiki.
Amos
Kaguta amefariki akiwa katika Hospitali ya Kimataifa ya Kampala, alikokuwa
amelazwa kwa siku kadhaa kwenye Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU).
Baba
huyo wa Rais, alikimbizwa hapo kutokana na matatizo ya tumbo aliyokuwa nayo, na
kulazimisha familia yake kumkimbizia hapo kwa matibabu zaidi.
Rais Museveni |
“Rais
Museveni na familia yote ya Kaguta, inasikitika kutangaza kifo cha baba yao
mpendwa Mzee Amos Kaguta, 96, ambacho kimetokea leo Februari 22 saa 1 asubuhi
kwenye Hospitali ya Kimataifa ya Kampala.
“Familia
inawashukuru madaktari wote kwa kujitoa na kupigania maisha ya Mzee Kaguta hadi
umauti ulipomkuta.
“Taarifa
zaidi juu ya mazishi yake zitatangazwa baadaye. Apumzike kwa Amani Mzee
Kaguta,” ilisomeka taarifa fupi kutoka kwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya
Habari Ikulu, Lindah Nabusayi Wamboka.
Daktari
wa familia, Diana Atwine alisema kuwa Mzee Kaguta alikimbizwa Hospitali baada
ya kuanza kulalamika mamumivu ya tumbo, huku habari nyingine zikieleza kuwa
marehemu alikuwa na matatizo ya kichwa.
Imeelezwa
pia kwamba, Rais Museveni alikuwa akitembelea mara kwa mara hospitalini hapo,
kujua maendeleo ya hali ya baba yake, hadi kifo kinamfika.
Kifo
cha Amos Kaguta, kinamuacha Rais Museveni bila wazazi, baada ya mama yake mzazi
Esteri Kokundeka kutangulia mbele ya haki mwaka 1997.
Mungu alitoa, Mungu ametwaa – Jina lake lihimidiwe, pia
ailaze roho ya marehemu mahali pema PEPONI, Ameen.
No comments:
Post a Comment