Tanzania
imeahirisha ombi la kuuza zaidi ya tani 100 za pembe za ndovu ili kuendana na
kanuni zilizowekwa na Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama na Viumbe
Vilivyo Hatarini (CITES).
Tanzania
itaongeza udhibiti dhidi ya uwindaji haramu na kuimarisha vikwazo vya magendo
ya pembe za ndovu kabla ya kutuma tena ombi lake. Serikali pia itafanya sensa
ya idadi ya tembo kujua kiwango cha wanyama hao nchini humo, kwa mujibu wa
taarifa ya Wizara ya Utalii na Maliasili.
Tanzania
imeomba kuuza pembe za ndovu zilizomo kwenye ghala yake, zilizopatikana
kutokana na tembo waliokufa vifo vya kawaida au waliouliwa kwa sababu ya
kuhatarisha maisha ya wanadamu, ili kugharamia vyema programu zake za ulinzi wa
rasilimali.
CITES
ilikataa ombi kama hilo la serikali ya Tanzania mwaka 2010, ikihoji kwamba
kuzipeleka pembe hizo sokoni kungeliongeza, na sio kupunguza, visa vya uwindaji
haramu.
No comments:
Post a Comment