CHAMA cha Aliance For Democratic (ADC) kimemwonya
Katibu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kwamba iwapo ataendelea kukishambulia
majukwaani, kitaanika maovu yake yote aliyoyafanya ndani ya chama chake na Watanzania
kwa ujumla.
Kimeeleza
kushangazwa kwake na kitendo cha Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar, kutumia majukwaa kuwashambulia viongozi wa ADC badala ya
kueleza sera za CUF na mustakabali wa matatizo yanayowakabili wananchi.
Onyo
hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa ADC, Said Miraji alipohutubia
wakazi wa Tanga kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Tangamano, mjini hapa.
Kwa
mujibu wa miraji, miongoni mwa kashfa mbaya za Malim Seif ni kubadilisha
makubaliano ya muundo wa Serikali ya Umoja Zanzibar ambayo yalitiwa saini na
Hamad Rashid kwa upande wa CUF na Kingunge Ngombare- Mwiru kwa CCM.
Alidai
kuwa makubaliano hayo yalikuwa yakieleza mgawanyo wa madaraka uanzie ngazi ya
taifa hadi shehia.
“Badala
yake, ameweka mawaziri watano tu kupitia CUF, je hiyo ni Serikali ya Umoja
kweli au kuwageuka wanachama wake kwa kukubali kufunga ndoa na CCM,” alisema
Miraji.
Mwenyekiti
huyo aliambatana na Mlezi wa ADC Kanda ya Kaskazini, Doyo Hassan Doyo, Mlezi wa
Kanda ya Pemba, Shoka Khamis Juma na Masaga Masaga ambaye ni Kamishna wa Kanda
ya Pwani.
Miraji
alisema ni jambo la kushangaza kuona Maalim Seif kusimama majukwaani kukisakama
chama kichanga kama hicho, badala ya kutumia nafasi yake na uzoefu
kuviunganisha vyama vya upinzani.
Alisema
sera ya ADC siyo kukisakama chama chochote cha upinzani ikiwamo CUF, bali ni
kuhakikisha vinashirikiana kikamilifu kukiondoa madarakani CCM.
Kuhusu
Katiba ya ADC, Miraji alisema ni chama pekee chenye katiba nzuri tofauti na
vyama vingine vyote, kwani inatambua uwapo wa Mwenyezi Mungu na imeweka ukomo
wa muda wa uongozi kuwa vipindi viwili.
Alisema katiba yao inatambua na kuweka mbele maslahi ya walemavu, inaelezea itakapopata ridhaa ya kuongoza nchi mwanaume aliyemuoa mwanamke mlemavu atasaidiwa na serikali.
No comments:
Post a Comment