Aliyekuwa Msanii maarufu katika tasnia ya filamu nchini Juma Kilowoko (SAJUKI) enzi za uhai wake kabla ya kukumbwa na maradhi. |
SAJUKI enzi za uhai wake baada ya kuwa amekwishaanza kusumbuliwa na maradhi |
Msanii Sajuki akiwa hospitali akiendelea kupata matibabu kutokana na tatizo la kupungukiwa damu. |
Aliyekuwa Msanii maarufu katika Tasnia ya Filamu
nchini Juma Kilowoko almaarufu kama ’SAJUKI’ aliyekuwa akisumbuliwa na
maradhi ya muda mrefu amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwa Katibu wa chama cha
waongoza filamu wilaya ya Ilala Bw. Rajabu Amiri amesema kuwa marehemu alikuwa
akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu hivi karibuni.
Maxmillian Kattikiro Blog: Inaungana na Familia ya
Marehemu pamoja na Watanzania wote katika Kuombeleza Kifo cha Mpendwa wetu
Marehemu SAJUKI… Inalilahi Wainalilahi Rajiun.
TAARIFA ZAIDI ZITAKUJIA HAPO BAADAE. ENDELEA
KUPERUZI Maxmillian Kattikiro Blog.
No comments:
Post a Comment