SPIKA wa Bunge Anna Makinda,
amempongeza Mbunge wa Arusha Mjini, Goodbless Lema (CHADEMA) kwa kurejea bungeni.
Spika alitoa pongezi hizo jana ndani ya
Ukumbi wa Bunge baada ya kumuona mbunge huyo akiingia ukumbini na kuketi kwenye
kiti chake.
“Naona Mheshimiwa Lema anaingia.
Nachukua nafasi kukupongeza kwa kurudi bungeni. Karibu sana,” alisema spika
huku wabunge wengine wakishangilia kwa kupiga makofi.
Lema, mmoja wa wabunge machachari wa
CHADEMA, alikuwa nje ya Bunge kwa takribani miezi kumi baada ya Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha kumvua ubunge.
Kesi dhidi yake ilifunguliwa na
wanachama sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao pamoja na mambo mengine
walidai Lema alimkashifu mgombea wao, DkBatilda Burian.
Hata hivyo, Lema alikata rufaa na
kurejeshewa ubunge wake Desemba mwaka jana.
Tayari Lema ameahidi kufufua hoja zote
alizoziacha bungeni, ikiwemo hoja kwamba Waziri Mkuu alilidanganya Bunge.
No comments:
Post a Comment