To Chat with me click here

Thursday, January 31, 2013

TUME YA KATIBA YAKAMILISHA KUPOKEA MAONI MAKUNDI MAALUM


Tume ya Mabadiliko ya Katiba imefunga rasmi kupokea maoni ya uundwaji wa katiba mpya kutoka kwa makundi, taasisi na watu wenye hadhi ya kitaasisi.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, alipozungumza na NIPASHE.

“Upokeaji wa maoni kwa njia nyingine bado unaendelea, isipokuwa tumefunga kupokea maoni kutoka kwa watu,” alisema Jaji Warioba.

Tume hiyo iliapishwa na Rais Jakaya Kikwete Aprili 13, mwaka jana na kuanza kazi ya kukusanya maoni  Julai 2, mwaka jana, baada ya kujigawa katika makundi saba.

Tume hiyo Ilipewa muda wa miezi 18 kufanya kazi hiyo hadi Aprili 26, mwaka 2014.

Tume ilijipangia kufanya kazi yake kwa awamu mbili tofauti; awamu ya kwanza ikiwa ni kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi na awamu ya pili itakuwa ni kuandaa taarifa, mapendekezo na rasimu ya Katiba Mpya.

Baadaye Tume itakutana na Mabaraza ya Katiba,  na mwishowe rasimu ya katiba itafikishwa kwenye Bunge Maalum litakalowakilishwa na makundi mbalimbali katika jamii.

Baada ya hapo itaitishwa kura ya maoni, ambayo itatoa fursa kwa wananchi kuamua kama wanairidhia rasimu ya katiba hiyo au la.

Tume hiyo ina wajumbe 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiongozwa na Jaji Warioba (Mwenyekiti) na Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (Makamu Mwenyekiti).

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment