TUME
ya Mabadiliko ya Katiba, jana ilianza kukusanya maoni ya vyama vya siasa katika
mchakato wa Katiba Mpya, huku baadhi ya vyama hivyo vikitoa mapendekezo
mbalimbali kuhusu suala la urais.
Vyama
vilivyozungumzia urais katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam
ni CCM, CUF na Chadema.
Taarifa
za vyama hivyo zilipatikana baada ya wawakilishi wao kuwasilisha maoni kwenye
tume hiyo katika mkutano wa ndani ambao waandishi wa habari hawakuruhusiwa
kuingia.
Wakati
CCM ikitaka Katiba ijayo iruhusu mgombea binafsi, Chadema imependekeza
Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 aruhusiwe kupiga kura na
kugombea nafasi yeyote ya uongozi nchini. CUF imependekeza Muungano wa Mkataba.
Mwanasheria
wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema chama
hicho cha upinzani, kimependekeza Katiba Mpya imtambue mtu mwenye umri wa
kuanzia miaka 18 kuwa ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kushika nafasi yoyote
ya uongozi nchini.
“Haingii
akilini kwa mtu mwenye umri wa miaka 18 anakubalika kupiga kura na kumchagua
kiongozi anayemtaka, lakini yeye mwenyewe hakubaliki kugombea nafasi yoyote ya
uongozi ikiwamo urais, ubunge na udiwani,” alisema Lissu.
Alihoji
“Kama Katiba ya sasa inamtambua mtu mzima kuwa ni yule anayeanzia umri wa miaka
18, kwa nini linapokuja suala la kuchaguliwa kwa ngazi zote ananyimwa haki hiyo
hata kama ana vigezo vingine?”
Pia Lissu alisema kuwa Katiba Mpya haina budi kuanzisha utawala wa majimbo yasiyozidi kumi ili kuleta uwiano katika matumizi ya rasilimali kwenye maeneo yote ya nchi.
Aliyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Nyanza Magharibi ambalo litajumuisha mikoa ya Kagera, Geita na Shinyanga; Nyanza Mashariki mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu, Ziwa Tanganyika kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa na Jimbo la Kati litakalojumuisha mikoa ya Dodoma, Tabora, Singida na Iringa.
Mengine
na mikoa yake kwenye mabano ni Jimbo la Kaskazini ( Arusha, Manyara na
Kilimanjaro), Pwani ya Kaskazini (Tanga, sehemu za Pwani na sehemu za
Morogoro), Jimbo la Dar es Salaam, Jimbo la Pwani Kusini (Mtwara, Lindi, Wilaya
za Mafia, Rufiji na Ulanga) na Kanda ya Nyanda za Juu (Njombe, Mbeya na
Ruvuma).
Mwakilishi
wa CCM, Andrew Chenge alipendekeza kuwapo kwa mgombea binafsi katika nafasi
zote ili kutoa fursa ya wananchi wasio wanachama wa chama chochote cha siasa
kupata nafasi ya uongozi.
Alisema,
kitakachofanyika ni kitengeneza mazingira mazuri ambayo yatawezesha mgombea
huyo kupatikana bila ya kuwapo kwa itikadi za udini au ukabila.
“Mapendekezo
ya chama chetu ni kuwapo kwa mgombea binafsi ili kushiriki kwenye nafasi zote
za uongozi. Hii itasaidia kuondoa ubaguzi au kuleta udini, jambo ambalo
linaweza kutoa fursa kwa wananchi wasio na udini wala chama kushiriki kwenye
nafasi ya uongozi,”alisema Chenge.
CUF Serikali tatu
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa, chama hicho, kimependekeza kuwa na mkataba katika masuala mbalimbali yanayohusu Muungano.
No comments:
Post a Comment