A.
JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE
1.
Kutakuwa na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya
Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya
kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki
hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano
lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni (referendum/plebiscite)
kwa idadi isiyopungua theluthi mbili ya kura zote halali.
3.
Kutakuwa na Serikali ya
Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee. Mambo ya
Muungano yatakuwa yafuatayo:
(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa;
(b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza;
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic);
(d) Uraia na uhamiaji;
(e) Sera za fedha na sarafu;
(f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha;
(g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.

4. Kutakuwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi
na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya
Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la
Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.
6. Rais wa Jamhuri ya
Muungano atachaguliwa kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na anaweza
kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano, na atachaguliwa kwa
msingi wa kuachiana zamu ya kushikilia madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
Kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.
No comments:
Post a Comment