To Chat with me click here

Wednesday, June 6, 2012

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WALA KIAPO

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hilo.Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charles Kizigha, Mhe. Maryam Ussi Yahya, Mhe. Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt. Twaha Issa Taslima,Mhe. Abdullah Ali Hassani Mwinyi, Mhe. Bernard Musomi Murunyama, Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta,anaeingia kwa uwadhifa wake wa uwaziri.
 Wabunge wameapishwa pamoja na wabunge wenzao wa Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi.

No comments:

Post a Comment