Mh. Zitto Kabwe akiwasili viwanja vya Bunge kuwasilisha bajeti ya Upinzani.
Mh. Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli.
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge
wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo
kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya
ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo
ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo
tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama
inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
MAPATO |
SHILINGI MILIONI
|
||
A | Mapato ya ndani |
|
11,889,078
|
i)mapato ya kodi (TRA) |
10,232,539
|
|
|
ii)Mapato yasiyo ya kodi |
1,163,533
|
|
|
B | Mapato ya Halmashauri |
493,006
|
|
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa
ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa
Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii
inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012
No comments:
Post a Comment