Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ameibua ufisadi unaodaiwa
kufanywa katika mgodi wa Kiwira na kulitaka Bunge kuunda kamati maalumu
ya uchunguzi.
Mkono alidai kuwa sehemu moja ya mgodi huo yenye utajiri mkubwa imeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa kampuni moja ya Australia.
Alisema uuzaji huo ni kinyume cha makubaliano yaliyofikiwa na Bunge
mwaka 2007 ambapo liliagiza kuwa mgodi wa Kiwira uliokuwa umeuzwa kwa
Kampuni ya Tan Power urudishwe serikalini baada ya kuwa umeuzwa kwa dola
laki saba tu.
Hata hivyo, Mkono alisema kuwa katika hali ya kushangaza Kampuni ya
Tan Power ambayo ilikuwa imeingia ubia na serikali iliuzwa kwa
Waustralia kiasi cha mabilioni ya dola. “Mheshimiwa Spika, Kiwira kulikoni? Lini Bunge litaunda kamati ya
kwenda kuangalia Kiwira?” alihoji na kusema kuwa pamoja na yote hayo,
sasa serikali imetenga sh bilioni 40 kwa ajili ya mradi wa Kiwira na
kuhoji nani aliteketeza fedha za awali zilizotolewa kwa ajili hiyo.
No comments:
Post a Comment