Bajeti ya Mwaka huu 2012/2013 ni Bajeti ya Madeni
Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) 
katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba 
mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;
1    Huduma kwa Deni la Taifa              Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2    Wizara ya Ujenzi.                             Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3    Wizara ya Ulinzi                               Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4    Wizara ya Elimu                               Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5    Wizara ya Nishati na Madini          Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
  TOTAL                                              TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo 
asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye 
kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni 
malipo kwa Deni la  Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa 
Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya 
miaka ya nyuma.
Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya 
kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa 
maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) 
zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni 
mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha 
uliopita.
Wabunge wanapaswa kufanya uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu 
inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa sana ya kuharakisha 
kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti
 ili kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa 
wabunge ili kuwezesha kuboresha Bajeti.
Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi
 sasa ithibitishwe na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza 
udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi na pia Deni la Taifa.


 
 
No comments:
Post a Comment