To Chat with me click here

Tuesday, June 12, 2012

WANANCHI WA MAJUMBA SITA WAFUNGA BARABARA YA PUGU KWA MASAA 4

Wananchi wa maeneo ya Majumba Sita karibu kabisa na kambi ya jeshi la wananchi Tanzania upande wa Anga (Airwing) leo walilazimika kufunga barabara ya Pugu kwa takribani muda wa masaa 4 hivi, kwa kile walichodai kuwa, wamechoshwa na vifo ambavyo hutokea mara kwa mara kutokana na magari kugonga wananchi wa maeneo hayo wengi wao wakiwa vijana ambao ndio tegemeo na nguvu kazi ya taifa. 
Wananchi hao walilalamika kuwa, mwanzoni barabara hiyo kabla ya upanuzi wake, ilikuwa na matuta ambayo yaliweza kudhibiti mwendo kasi wa magari, lakini tangu upanuzi wa barabara ulipofanyika hakukuwekwa matuta wala alama za vivuko vya wenda kwa miguu (Zebra Cross) hivyo kupelekea ajili nyingi kutokea. 

Wakizungumza na mwandishi wetu, watu hao wamesema kuwa katika wiki moja huweza kuzika watu watatu mpaka wanne kutokana na ajali hizo. Wakidhibitisha madai hayo waliongeza kuwa, tangu jumamosi ya tarehe 9, june hadi kufika leo tarehe 12 wameshazika watu 3 kutokana na ajali za barabarani hapo. 

Akiojiwa na mwandishi wetu, mwenyekiti wa serikali za mtaa wa majumba sita Bibi. Rukia Chacha maarufu kama mama Ng'ombe, amesema kuwa, wamekuwa wakiomba ujengwaji wa matuta wa sehemu hiyo kwa muda mrefu lakini wahusika wamekuwa wakipuuzia na kusababisha vifo kila kukicha. "Nimekuwa nawasiliana na wahusika pamoja na Tanroads, lakini hakuna utekelezwaji wa ahadi zao za kuwa wanakuja, sasa nashangaa kwanini serikali inalichukua swala hili kirahisi hivyo" kama alivyonukuliwa.   
Bibi. Rukia Chacha (Mama Ng'ombe) akizungumza na waandishi wa habari
Kamanda wa polisi wa wilaya naye alikuwepo kuhakikisha kuwa kero za wananchi hao zinasikilizwa na kutekelezwa. Akihojiana na mwenyekiti huyo wa mtaa, kamanda huyo alisema kuwa ni nvyema wananchi wakaachia barabara ili shughuli nyingine za kimaendeleo zisikwame, lakini bila mafanikio, wananchi walizidisha mgomo huo huku wengine wakiwa wamelala barabarani wakidai kuwa walikuwa wakimuitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Mhe. Mecky Sadick ili kujadili swala hilo pamoja nao.
Kamanda wa polisi wa wilaya akihojiwa na vyombo vya habari
Katika hali ya kustajaabisha mgomo huo uliodumu takribani kwa masaa manne, haukuweza kuruhusu yeyote kupita katika barabara hiyo kwani hata askari wa Magereza hawakuweza kuruhusiwa kupita bila kujali kuwa walikuwa na wafungwa hivyo kuwafanya walazimike kuweka doria kwa wafungwa hao hapohapo katikati ya barabara. 
Askari wa Magera wakiwa katika doria ya lazima katika mgomo huo.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wameketi katikati ya barabara kuonesha kuwa wanakerwa na vifo vya ndugu zao kila kukicha katika barabara hiyo.
Askari polisi na wale wa kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU) hawakuwa na lakufanya ila kusikila na kusubiri kuona na kutekeleza mahitaji ya wananchi ya kuonana na Mkuu wa Mkoa. 
Baadhi ya Mabango yaliyobebwa na wananchi ili kuishinikiza serikali kutekeleza maagizo yao. 
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama katikati ya barabara hiyo wakijadili jambo wakati mgomo huo ukiendelea
Kijana mmoja aliyewekwa chini ya ulinzi kwa tuhuma ya kurusha jiwe ambalo halikuleta madhara. kijana huyo aliachiwa muda mfupi baadaye baada ya wananchi kuwalazimisha askari hao kumwacha huru.
Misururu mikubwa ya magari, kama ionekanavyo katika picha kutokana na mgomo huo wa leo. 
Mpaka tunaondoka katika maeneo ya tukio, mgomo huo ulikuwa ukiendelea na bado wananchi walikuwa wakishinikiza kukutana na mkuu wa mkoa ili kujadili na kupata suluhu ya tatizo hilo.



No comments:

Post a Comment