To Chat with me click here
CHADEMA UKONGA TISHIO KWA CCM - JIMBONI
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Ukonga kinayo heshima
kubwa sana kuwataarifu ndugu Wananchi wa Jimbo la Ukonga kwa ushirikiano
mkubwa waliouonesha wakati wa Mikutano ya hadhara ambapo chama-Jimbo
kilipokea takribani wanchama 50 toka CCM na vyama vingine.
Chama –
Jimbo la Ukonga kimekuwa kikiendea kufanya mikutano ya hadhara kwenye
kata mbalimbali na kuwapokea wanaCCM wengi na kufanya ongezeke la
wanachama wapya kuwa kubwa mno hivyo kukipelekea Chama Jimbo kukosa
uwezo wa kuendelea kuendesha mikutano ya hadhara pia kukabiliana na
ongezeko hilo, ingawa kuna taratibu na harakati ambazo tunaendelea nazo
ili kuhakikisha tunawakaribisha vyema wanachama hao wapya na kuongeza
kasi ya mapambo ili kuendelea kupata wanachama wengi zaidi.
Mpaka sasa tumeshafanya mikutano na kupokea waliokuwa wanachama wa CCM
katika kata za Kitunda, Ukonga, Chanika na Majohe. Vilevile tunategemea
tarehe 03/06/2012 kufanya mkutano mwingine mkubwa wa kuwapokea wanachama
wapya wanaotokea CCM na vyama vingine katika kata ya Pugu, na mpaka
sasa kuna matawi matatu ya CCM kata ya Ukonga na Kivule ambayo
yamekwisha omba kutaka mikutano ya hadhara ili wasalimimshe kadi na
uanachama wa CCM kwa viongozi wa Chadema Jimbo.
Ni imani yetu
sisi wanaCHADEMA-Ukonga na viongozi wake kuwa, sasa kazi imeanza na
hakuna kulala mpaka kieleweke maana kwa utaratibu huu unaoendelea kwenye
chama uongozi wa Taifa, tunaamini kuwa kata na majimbo mengine mengi
yatafuata mwenendo huu kwani wamekuwa wakionesha ari hiyo ya kukihama
chama tawala.
27/05/2012 CHADEMA tumepokea wanachama zaidi ya
hamsini (50) na uongozi mzima wa matawi wa kata ya Majohe, ambao
wamejiunga na chama chetu. Zipo taarifa zaidi kuwa kuna matawi mengine
mawili ya chama cha mapinduzi (CCM) yamepania kujiunga na CHADEMA hivi
karibuni tena kwenye moja ya mikutano ya hadhara ambayo tunategemea
kuifanya.
Hivyo tunawaomba wananchi wote wenye mapenzi mema na
chama (CHADEMA) na wenye uzalendo wa kutosha kutuunga mkono katika
jitihada zetu za ukombozi wa nchi toka kwenye makucha ya wajanja
wachache ili kuleta maendeleo ya kweli na maisha bora kwa umma wa
watanzania, ili tuweze kufikia malengo hayo kwa urahisi zaidi.
Tunakaribisha michango yenu ya hali na mali hata mawezo yenu ya
kuboresha na kukiimalisha chama zaidi katika hili.
Wenu katika ujenzi wa Taifa/Chama
Kny. Katibu Jimbo la Ukonga.
Maxmillian Kattikiro.
No comments:
Post a Comment