Mchakato wa Bajeti katika
Serikali za Mitaa
Tanzania Bar inazo wilaya 133,
manispaa, majiji na miji. Hii huunda Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local
Government Authorities), na kila mamlaka ina halmashauri yake iliyochaguliwa.
LGA husaidia kutoa huduma za jamii kama vile elimu, huduma za afya, upatikanaji
wa maji vijijini, kilimo na barabara. Wajumbe
wa halmashauri yaani madiwani huchaguliwa na wananchi na hukuwakilisha
wewe pamoja na mahitaji yako. Ni wajibu wao kutetea mahitaji yako pamoja na
kupigania haki zako kwenye vikao vya halmashauri. Wanawajibika kukupatia
taarifa zote muhimu.
Nani
anawajibika katika mchakato wa Bajeti ya serikali za mitaa?
Wadau mbalimbali wanahusika katika
mchakato wa bajeti ya serikali za mitaa kama inavyooneshwa hapa chini.
·
Mkutano
Mkuu wa Kijiji
·
Halmashauri
ya Kijiji
·
Baraza
la Kata
·
Wakurugenzi
wa Halmashauri / Viongozi wa Halmashauri
·
Sekretarieti
ya Mkoa
·
Serikali
Kuu
·
Ofisi
ya Waziri Mkuu TAMISEMI
Wizara katika ofisi ya waziri mkuu
TAMISEMI huandaa sera na miongozo inayosimamia uendeshaji wa serikali za mitaa.
Serikali kuu kupitia wizara husika
(Kama vile Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii) huandaa sera zinazosimamia sekta
zinazohusika.
Sekretarieti ya mkoa chini ya
usimamizi wa Afisa Tawala wa mkoa (Regional Secretariate) huunganisha serikali
kuu na mamlaka za serikali za mitaa. Sekretariati ya Mkoa hutoa taarifa za
miongozo ya namna ya kupanga, kuandaa bajeti pamoja na utekelezaji wake.
Katika ngazi ya serikali za mtaa,
Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na uongozi wa Halmashauri husimamia
utekelezaji wa bajeti kama ilivyopangwa. Halmashauri (inayojumuisha madiwani na
wabunge) huijadili bajeti pamoja na kuikubali au kuipitisha.
Kamati ya maendeleo ya Kata (Ward Development
Committee) Ni kiunganishi kati ya vijiji, vitongoji na halmashauri ya wilaya.
Wajumbe wa kamati hii hujumuisha diwani wa kata, afisa mtendaji wa kata na
wenyeviti wa vijiji. Kamati ya maendeleo ya Kata (WDC) hukutana kila baada ya
miezi mitatu. Pia inaweza kukutana mara nyingi zaidi kama itaonekana kuna
umuhimu wa kukutana.
Halmashauri ya Kijiji (Village Council)
inahusisha Mwenyekiti wa kijiji au kitongoji pamoja na viongozi wengine
wanaochaguliwa na mkutano mkuu wa Kijiji.
Mkutano mkuu owa Kijiji hujumuisha wanawake na wanaume wenye miaka 18 na kuendelea.
Kila mwanakijiji aliye mtu mzima humiliki Mali za Kijiji kama vile ardhi,
misitu na njia za usafiri wa majini. Kwa mujibu wa sheria, halmashauri ya
kijiji inapaswa kukutana walau mara nne kila mwaka. Kwa upande wa majiji,
manispaa na miji kuna baraza la manispaa na mtaa.
Fedha
zinatoka wapi?
Fedha katika bajeti za mitaa
zinapatikana kutokana na vyanzo viwili: Mapato ya nje na mapato ya ndani.
Mapato
ya nje:
Hizi ni fedha kutoka serikali kuu
ambazo ni karibu asilimia 90 ya bajeti nzima ya serikali za mitaa. Vyanzo vya
mapato hayo ni vya aina tofauti tofauti.
Ruzuku
Kila halmashauri inapewa ruzuku na
serikali kuu kwa ajili ya matumizi ya kawaida (ambayo hujumuisha malipo ya
mishahara pamoja na gharama zingine za uendeshaji) katika kila sektabmuhimu ya
kijamii (afya, elimu, maji katika vijiji, kilimo na barabara) pamoja na ruzuku
ya uendeshaji. Ruzuku inapaswa kutumika kama ilivyoelekezwa na serikali kuu na
si vinginevyo. Kwa wastani asilimia 60 ya bajeti ya serikali za mitaa
inategemea ruzuku.
Mfuko wa fedha kwa ajili ya sekta
maalumu
Hizi ni fedha za ziada za matumizi ya
kawaida zinazotolewa kulenga sekta Fulani muhimu zilizopo chin ya wizara
husika. Kwa mfano fedha kwa ajili ya
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) na fedha kwa ajili ya Mfuko wa
pamoja wa huduma za afya (Healthy Sector Basket Fund). Fedha hizi hutolewa ili kusaidia maendeleo ya
kilimo pamoja na huduma za afya. TACAIDS hutoa fedha katika halmashauri zote
kwa ajili ya kugharamia miradi ya VVU/UKIMWI.
Fedha
kupitia mkakati wa uchumi na kuondoa
umaskini Tanzania
(MKUKUTA)- fedha hizi hutolewa kwa
ajili ya shughuli za maendeleo zikilenga kupunguza umasikini. Fedha hizi kwa
kawaida zinatumika kuboresha miundombinu pamoja na vipaumbele vingine
vilivyowekwa na halmashauri. Piafedha hizi hutumika kujenga uwezo wa serikali za mitaa pamoja na shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa, huduma za afya, miradi ya maji vijijini, ujenzi wa
barabara mpya n.k.
Vipaumbele vinapangwa na wewe
mwananchi wakati mchakato wa kuainisha fursa na vikwazo vya maendeleo (Opportunity and Obstacles to Development). Kwa
wastani, fedha hizi huchukua asilimia 17 ya bajeti nzima ya mwaka ya
halmashauri.
Misaada
maalumu ya maendeleo-misaada
hii kwa kawaida hulenga mikoa, sekta au maeneo maalumu na ina malengo maalumu.
Kwa mfanomradi wa uwezeshaji katika kilimo (PADEP), mradi wa uwekezaji katika
kilimo ngazi ya wilaya (GASIP), mradi wa Hifadhi ya Mazingira na maendeleo ya
mji (UDEM), mradi wa ushirikishwaji katika maendeleo ya misitu (Participatory Forest Management), mradi wa
uhifadhi wa ardhi endelevu (Sustainable Wetland Management), Ruzuku ya
usafirishaji katika wilaya na vijiji (LGTP/VTTP), Ruzuku ya maendeleo ya
Halmashauri na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEE. Fedha hizi
huchangia wastani wa asilimia 5 ya bajeti ya mwaka ya serikali za mitaa.
Fedha za ziada
Fedha zingine pia katika halmashauri
utolewa na washirika wa maendeleo, miradi na mipango maalum ya serikali au
michango ya watu binafsi. Halmashauri ya Kijiji (VC) inapaswa ifahamu kuhusu
fedha hizi.
Mapato
ya ndani:
mapato haya hupatikana ndani ya wilaya na kwa kawaida huwa ni asilimia 10 ya
bajeti nzima.
Kodi za serikali za mitaa: Serikali
itaa vile vile hupata fedha kutokana na kodi mbalimbali zinazotozwa. Taarifa
hiyo hapo chini inaorodhesha vyanzo hivyo vya mapato. Kwa wastani, kodi hizi
huchangia asilimia 8 ya bajeti zao za mwaka.
Mapato ya ndani ya serikali za mitaa
Kodi za vitu
·
Kiwango
Kodi kwenye
vitu vya huduma
·
Ushuru
wa mazao (Kiwango cha juu ni 5% ya bei ya shambani)
·
Ushuru
wa mazao ya misitu
Kodi kutokana
na za utaalamu
·
Ushuru wa nyumba za kulala wageni
Leseni za
biashara na za utaalamu
·
Ushuru wa uvuvi wa kibiashara
·
Ushuru
wa leseni kwa huduma binafsi ya afya
·
Ushuru
wa leseni za teksi
·
Ushuru
wa leseni ya usafirishaji mizigo
·
Ushuru
wa leseni nyingine za biashara
Magari
·
Ushuru wa leseni za magari
·
Ushuru
wa leseni ya vyombo vya uvuvi
Kodi zingine
kwa ajili ya matumizi ya vitu, ruhusa kutumia vitu.
·
Ushuru
wa leseni za bidhaa za misitu
·
Ushuru
wa uchimbaji wa vifaa vya ujenzi
·
Ushuru
wa leseni za uwindaji
·
Ushuru
wa leseni ya kumiliki silaha
·
Ushuru
wa matangazo
Kodi za mapato
·
Ushuru
wa huduma
Mapato
yatokanayo na umiliki wa vitu pamoja na
shughuli za ujasiliamali
·
Gawio
·
Mapato
mengine ya ndani na miliki
·
Riba
·
Ukodishaji
ardhi
Vyanzo vingine
vya mapato
·
Ada
za shughuli za kiutawala
·
Faini,
adhabu na mali zinazotelekezwa
MAMLAKA
ZA SERIKALI ZA MITAA HAZIRUHUSIWI KUTOZA KODI YA AINA YOYOTE AMBAYO HAIPO
KWENYE ORODHA HII
Michango ya jamii
Hii ni ya jamii nzima.
Kutegemeana na aina ya miundombinu, mfano darasa, michango hii inaweza kuwa na
tofauti kati ya asilimia 2.5 hadi 30 ya gharama zote ingawa mara nyingi ni
asilimia tano. Michango hii inatakiwa itumike kwa ajili ya kuendeleza miundombinu
ambayo
imepewa kipaumbele na jamii kupitia
zoezi la utambuzi wa fursa na vikwazo vya maendeleo
(O & OD).
Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)
Huu ni mpango wa ubia kati ya serikali
na Benki ya Dunia unaolenga kutoa fehda kwa ajili ya miradi ya miundombinu
pamoja na kutoa ajira za muda mfupi. Ubia huu umelenga kuwashirikisha wananchi
katika Nyanja za barabara, kupitia mipango ya maendeleo ya jamii ikilenga
kuboresha huduma za jamii kama vile maji au mpango wa jamii unaolenga kutoa
huduma kwa makundi yanayoishi mazingira hatarishi, kwa mfano kutoa mafunzo kwa
watu wenye ulemavu.
Mfumo huu ni mgumu, kwa mfano shule
inaweza kupokea fedha kutoka kwenye vyanzo vingi ambavyo ni tofauti kama
inavyoonesha hapo chini.
- Ruzuku
- GBS
- Ruzuku ya Ziada
- Fedha za Maendeleo
- MMEM
- Michango ya Jamii
- Local Government Capital Development Grant (LGCDG)
No comments:
Post a Comment