Msanii nyota wa filamu nchini,
Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo
linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zimepatikana
jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili
kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza
kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa
madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua
tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi
mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa
marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain
Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli
kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni
mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo
(cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa
mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo
limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa
kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa
na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa
kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa
ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na
ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki katika
uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji
huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa
upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu,
vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu
kingine katika mwili huo
No comments:
Post a Comment