To Chat with me click here

Wednesday, August 8, 2012

RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu,Rais Yower Kaguta Museveni wa Uganda mwishoni mwa mkutano huo uliomalizika leo jijini Kampala Uganda.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini maazimio ya wakuu wa nchi za Maziwa Makuu mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Speke’s Bay Resort,Munyonyo, KAMPALA, Uganda.

Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi wakimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea jijini Kampala Uganda ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wan chi za Maziwa Makuu.

M4C LONDON....LEMA ANENA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema, akitoa neno kwenye mkutano wa ufunguzi wa tawi la Chadema London jana usiku kama aonekanavyo pichani.

Tuesday, August 7, 2012

CAG AANZA KUCHUNGUZA MADUDU TANESCO

NI PAMOJA NA MADAI YA MATUMIZI MABAYA YA OFISI DHIDI YA MHANDO

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema ofisi yake imeanza ukaguzi wa tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando.

Julai 14 mwaka huu, Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco ilimsimamisha kazi Mhando na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi wa Ununuzi, Harun Mattambo kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Utouh aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba ofisi yake imekabidhiwa kazi hiyo na tayari imeshaanza na imefikia pazuri. “Ni kweli suala hilo nimeshakabidhiwa na kazi hii  tayari imeshaanza na imefikia pazuri. Kikao cha kwanza kimekaa Jumamosi iliyopita na mimi nimeshafika kuwahakiki maofisa wangu wanaoshughulikia hilo,” alisema Utouh na kuongeza kuwa kazi hiyo inaweza kukamilika ndani ya siku 60 kuanzia sasa.

WAZIRI MEMBE ABANWA


ATISHIA KUJIUZULU, SERIKALI YAFUNGA MJADALA, CHENGE SAFI

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisema hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemkalia kooni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakimtaka awataje watuhumiwa na kashfa hiyo.

Wabunge hao walitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa wakichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa na kwamba mbali na kutajwa kwa watuhumiwa hao pia serikali iwachukulie hatua na si kufurahia tu chenji yake ambayo imerejeshwa nchini hivi karibuni.

Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Mashishanga (Chadema), alisema kuwa Waziri Membe alipata kueleza anawafahamu watuhumiwa na kashfa hiyo ni vema akawataja, ili jamii iwatambue.

MNYIKA ‘AVALIA NJUGA’ SHERIA ZA HIFADHI YA JAMII

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika anakusudia leo kutangaza utaratibu wa kusanya saini za wabunge wasiopungua 10 ili kuunga mkono mpango wake wa kuwasilisha bungeni muswada binafsi wa marekebisho ya sheria za
hifadhi ya jamii ili kurejesha fao la kujitoa linalolalamikiwa nchini kote.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana, Mnyika alisema uamuzi huo umetokana na ushauri wa wabunge wenzake na maoni ya wafanyakazi aliyoyakusanya kwa njia mbalimbali ikiwamo ya mtandao Agosti 4 na 5 mwaka huu.

“Nitaeleza utaratibu wa kukusanya saini za hati ya dharura ya muswada baada ya mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira na majumuisho ya waziri husika,” alisema Mnyika.

Agosti 3, mwaka huu mbunge huyo alieleza kuwa mgogoro uliopo chanzo chake, mbali na marekebisho ya sheria yaliyofanyika Aprili 13, ni
tafsiri potofu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu marekebisho hayo, kuhusu fao la kujitoa.

Alisema tatizo kubwa halikuanzia katika marekebisho ya mwaka huu, bali ni udhaifu wa mfumo wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii ambao unahitaji marekebisho makubwa.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa muswada atakaowasilisha bungeni unahusu fao linalolalamikiwa na mambo mengine ambayo hakuyaweka wazi.

Katika siku za karibuni, kumekuwa na mjadala mkali kuhusu marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kufuta kifungu kinachoruhusu fao la kujitoa na kuzua malalamiko kwa wafanyakazi na wanaharakati nchi nzima, kuwa sheria hiyo imelenga kuwanyima haki.

Katika baadhi ya maeneo, hasa migodi imedaiwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wameanza kugoma na wengine kuacha kazi baada ya kubaini kuwa hawataweza  kupata fedha zao na mafao kabla ya kufikisha miaka 55 na kustaafu kwa hiyari au miaka 60 ya lazima.

NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI KIBAHA JIONI HII



Anaitwa Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .

Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani".

Monday, August 6, 2012

LEMA AIPELEKA CHADEMA LONDON

M4C LONDON.


ALIYEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amepeleka harakati za Movement For Change (M4C) zinazoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nchini Uingereza.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka London Uingereza, Lema alisema kuwa moja ya shughuli atakazofanya akiwa huko ni kufungua matawi ya CHADEMA.
“Nilipofika tu Watanzania wengi wanaoishi hapa walionyesha nia ya kutaka kuwa na tawi katika jiji la London na tutakuwa na mikutano kadhaa ya ndani ya kubadilishana mawazo,” alisema Lema.

Lema ambaye amepata kuwa mbunge machachari ndani ya Bunge la Muungano, alisema CHADEMA itatumia nafasi hiyo kupata mawazo ya Watanzania wanaoishi nje ambao mara nyingi hawakuwa na fursa ya kutoa mawazo yao.

“Ingawa nimekuja kwa shughuli binafsi, nitatumia nafasi hiyo kueneza harakati zetu za Movement For Change na kubwa zaidi kupata maoni na michango ya mawazo ya Watanzania wanapenda mabadiliko nchini,” alisema Lema.

Kutakuwa na mkutano wa ufunguzi  wa tawi la CHADEMA LONDON ambapo utafanyika siku ya tarehe 07/08/2012 na Mhe. Godbless Lema. Mkutao huo utafanyika THATCHED HOUSE PUB iliyopo BARKING majira ya saa 2 kamili usiku, siku hiyo ya Jumanne.

Tangu alipovuliwa ubunge na Mahakama, Lema amekuwa akiendesha mikutano mingi ya Movement For Change ambayo imekuwa na mafanikio makubwa nchini tangu harakati hizo zilipoanzishwa.

Hivi sasa CHADEMA inatarajia kuvamia mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kupitia harakati zao za Movement For Change.

WALIMU WATISHIA KUING’OA CCM


WAKATI walimu wakikubali kurejea kazini na kuendelea kutafakari amri ya mahakama, mkakati mzito unapangwa kuhakikisha hawakiungi mkono Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tangu kutolewa kwa kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba mgomo huo si sahihi na serikali yake haina uwezo kutimiza madai yao na kufuatiwa na uamuzi wa mahakama, walimu wamekuwa wakiangalia namna nyingine ya kuibana serikali.

Mwishoni mwa wiki, walimu katika wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, walikuwa na kikao kizito ambapo pamoja na mambo mengine, walipendekeza kuiangusha CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Katika mkutano huo ulioitishwa na uongozi wa Chama cha Walimu (CWT) na kufanyika katika ukumbi wa Afro Berch mjini Nansio Ukerewe, baadhi ya walimu ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliwataka wenzao waungane kuing’oa CCM kwa madai kuwa serikali inayoiongoza imeshindwa kusimamia maslai yao.

“Ndugu zangu walimu, walimu tusitarajie kupata maslai bora kama CCM itaendelea kushika dola. Hebu angalieni tangu tulipoanza mvutano na serikali chama hicho kimebaki kimya huku kikitambua matatizo makubwa yanayotukabili. Tuungane tufanye maamuzi magumu mwaka 2015,” alisema mwalimu huyo.

Huku akiungwa mkono na walimu wengi, mwalimu huyo bila kumung’unya maneno, alisema ingawa maadili ya utumishi wa umma yanazuia watumishi kushiliki siasa, lakini muda umefika kwa walimu kutumia ushawishi wao kuhakikisha mwaka 2015, CCM inang’oka madarakani.
Mwalimu huyo alisema, walimu wakiamua kwa wingi wao wanaweza kwani ndio wanaotumika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa uchaguzi.

Mwalimu mwingine aliungana na mwenzake kuishambulia CCM kwamba inalinda kundi dogo la wanasiasa wanaoneemeka na rasilimali za taifa huku Watanzania wengi wakikabiliwa na umaskini.

Mwalimu huyo pia aliushambulia mfumo wa mahakama kwamba hauko huru kwenye kutoa maamuzi, akitolea mfano uamuzi wa kesi yao kuwa ulikuwa na mkono wa serikali.
Kwa upande wake, Katibu wa CWT wilayani humo, John Kafimbi, alimlalamikia Rais Kikwete kuzungumzia kesi yao huku akijua fika kwamba suala hilo liko mahakamani.

Aliwataka walimu wajipongeze kwani katika kipindi cha mgomo, wamedhihirisha kwamba wakiamu wanaweza kupigania haki zao.

Jijini Dar es Salaam, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema Rais Kikwete ameudanganya umma kwamba serikali inahitaji asilimia 75 ya bajeti yake kuboresha maslahi ya walimu tu wakati kiasi hicho ni kwa ajili ya watumishi wote.
Mbali ya hilo, CUF imeitaka serikali kuacha kutumia mahakama kuzima madai ya msingi ya walimu bila kutafuta njia sahihi ya kutatua.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema katika mazungumzo yake na wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika Ikulu jijini Da es Salaam Agosti mosi, Rais Kikwete alichukulia madai ya walimu na kulinganisha na nyongeza ya wafanyakazi wote serikalini badala ya kuja na tamko la kushughulikia matataizo ya walimu.

“Rais anaposema tutatumia asilimia 75 ya bajeti kama tukitekeleza madai ya walimu hawatendei haki Watanzania waliomsikiliza kwani alitumia takwimu za wafanyakazi wote serikalini kama wataongezewa mishahara kwa kiwango hicho na kuyafanya ndiyo madai ya walimu,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema, ingawa CUF haiamini kama migomo ya wafanyakazi ndio suluhu la matatizo, inaamini walimu wana madai ya msingi na ya haki yanayopaswa kushughulikiwa na kupewa kipaumbele. Mwenyekiti huyo wa CUF alimshangaa Rais Kikwete kushindwa kueleza mikakati ya kutekeleza madai ya walimu ili kuwanusuru na hali ngumu ya maisha.

“Serikali isiyo na mipango kwa vyovyote vile haina uhalali wa kuwatumikia wakulima na wafanyakazi, na hali hiyo inaitia aibu serikali inayoamua kuwahadaa walimu kwa mambo yaliyo wazi,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema kuna fursa nyingi ambazo serikali ya CCM imeshindwa kuzitumia na kama zingetumiwa ipasavyo, leo kusingekuwa na madai ya walimu wala wafanyakazi wa kada nyingine.

“Kwa kweli elimu ya Tanzania itaendelea kuwa duni ikiwa mchezo huu wa kuwapiga danadana walimu utaendelea….vigogo wa CCM ambao watoto wao wanasoma katika shule za kimataifa na za kimombo, katu hawawezi kuwafikiria watoto wa maskini wasio na mbele wala nyuma,” alisema Prof. Lipumba.

Alibainisha kuwa lazima walimu watambue CCM haiko madarakani kutatua matatizo yao, hivyo ni vema wakaungana kuhakikisha chama hicho kinaondoka madarakani.
Hivi karibuni Mahakama Kuu divisheni ya kazi ilisitisha mgomo wa walimu kwa madai kuwa ni batili.

Mahakama hiyo iliamuru pande zote zinazotofautiana kurudi katika meza ya majadiliano kwa ajili ya kusaka suluhu.

Tanzania Daima.

Saturday, August 4, 2012

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YATUPIWA KOMBORA

JUKWAA la Katiba Tanzania na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), limeirushia kombora  Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba inafanya utani katika zoezi zima la kukusanya maoni ya wananchi jambo ambalo litasababisha ipatikane Katiba ya kundi fulani la watu na siyo wananchi.

Kwa nyakati tofauti Jukwaa hilo na LHRC wameeleza kuwa utani huo upo katika machapisho ya kuelimisha umma yanayotolewa na Tume hiyo na upungufu katika ukusanyaji maoni, wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza kutokuwa na mkalimani, vituo vya kukusanyia maoni kuwa vichache, ratiba za tume, vyama vya siasa kuingilia mchakato na wajumbe wa tume kuendelea na shughuli zao za awali.

Kauli hiyo imekuja ikiwa imepita wiki moja tangu tume hiyo kumaliza kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa minane, huku ikijipanga kuendelea na zoezi hilo katika mikoa mingine minane, wiki moja kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kuwa, mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi inayofanyika asubuhi inawafanya wananchi wengi kukosa nafasi ya kutoa maoni yao kwa kuwa wanakuwa katika shughuli mbalimbali.

“Ufuatiliaji wetu umebaini kuwa  mikutano inayofanyika asubuhi kuanzia saa 3 hadi saa 7 mchana inakuwa na watu wachache ikilinganishwa na mikutano inayofanyika kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 jioni,”alisema Kibamba.

Alisema kuwa , hali hiyo huwakumba hasa wananchi waishio vijijini  kwa kuwa muda huo wanakuwa katika shughuli za kilimo  na ujenzi na kusisitiza kuwa mkutano unatakiwa kufanyika mara moja kwa siku nyakati za jioni ili kila mwananchi ashiriki.

Alisema kuwa tatizo jingine waliloligundua ni tume hiyo kutokuwa na watu maalumu kwaajili ya kukusanya maoni ya watu wenye ulemavu hasa wenye ulemavu wa kuzungumza na kusikia.

“Tulitoa ushauri awali kwamba Tume itafute watalaamu kwa ajili ya kuwa na mawasiliano na watu wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza lakini haikuwa hivyo, matokeo yake wanapohudhuria mikutano wanashindwa kutoa maoni yao” alisema Kibamba.

Alisema hata vituo vya kukusanyia maoni vipo vichache na  vilivyopo vipo mbalimbali  jambo linalowafanya wananchi wanaoishi katika vijiji au kata ambazo tume hiyo haifiki, kushindwa kutoa maoni yao.

“Machapisho yaliyoandaliwa na Tume pia hayana ubora na yapo machache, hata vile vinavyoeleza Katiba kwa lugha nyepesi haviko sawa, ilitakiwa viandaliwe na wataalamu kutoka asasi mbalimbali nchini,” alisema Kibamba.

Alisema kuwa tume hiyo inatoa ratiba za mikutano yake katika kipindi kifupi na kuongeza kuwa mwezi huu tume hiyo inaanza tena zoezi la kukusanya maoni, lakini mpaka sasa haijatoa ratiba zake.

Alisema kuwa suala jingine ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini ni kitendo cha vyama vya siasa kuingilia zoezi la utoaji maoni, huku wanachama wake wakisafiri kila kituo ambacho tume hiyo hufika kukusanya maoni.

“Pia kulikuwa na tatizo la baadhi ya wajumbe wa tume kuendelea na shughuli zao za awali  na kuacha majukumu yao ya kukusanya maoni, pia wananchi wamekuwa wakitishiwa na wajumbe kwa kubanwa na kuulizwa maswali magumu wanapokuwa wanatoa maoni yao,”alisema Kibamba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, DK Hellen Kijo –Bisimba alisema, wamebaini  kuwapo kwa upungufu mkubwa haki za wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru.

Alisema muda wanaopewa wananchi wa kutoa maoni yao hautoshi, kwani hautoi nafasi ya kutosha ipasavyo kama inavyotakiwa.

“Muda uliopangwa na tume wa saa tatu kuanzia saa tatu mpaka saa sita mchana au saa nane mpaka saa kumi na moja jioni kwa kila mmoja kupewa dakika tano  za kutoa maoni hazitoshi na tume haipaswi kufanya hivyo,” alisema Bisimba na kuongeza:

“Muda wa asubuhi kutumika kukusanya maoni ni kuwanyima haki watu wengi kushiriki kutoa maoni yao kwani wakati huo wengi wanakuwa makazini.”

Bisimba alifafanua kwamba taarifa za kuwapo kwa Tume ya kukusanya maoni imekuwa finyu na kwamba hali hiyo imepelekea watu wengi kuacha kushiriki kutoa maoni.

“Kutokana na kukosekana kwa taarifa za kuwapo kwa Tume ya kukusanya maoni katika Kata kumekuwa na mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kutoa maoni yao jambo ambalo linawanyima haki wananchi kutoa maoni yao,” alisema.

Friday, August 3, 2012

RAIS KIKWETE ATOA KIFUTA JASHO CHA NG’OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
  Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa baada ya kufanyika kwa mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) CHASITISHA MGOMO NCHI NZIMA


Rais Chama cha Walimu nchini (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akitoa taarifa ya chama hicho

UONGOZI wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), umesitisha mgomo uliokuwa unaendelea nchini, hivyo kuwataka walimu kurejea kazini.
Rais wa chama hicho, Mukoba amesema wameamua kusitisha mgomo, baada ya kuingiwa na hofu ya viongozi wao wa juu kuhofiwa kukamatwa.

Thursday, August 2, 2012

TAMKO LA HAKIELIMU KUHUSU MGOMO WA WALIMU TANZANIA, AGOSTI 2012



CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kiliitisha mgomo kwa walimu wote nchini kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 mpaka kitakapowajulisha vinginevyo. CWT kinaona mgomo ndio njia sahihi itakayoishinikiza Serikali kutekeleza madai ya walimu na kuwaboreshea mazingira ya kazi walimu. Mgomo huu leo unafikisha siku ya nne mfululizo.

HakiElimu inatambua kuwa walimu wamekuwa na mgomo baridi kwa muda mrefu sasa. Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka jana ulibaini kuwa asilimia 40.6 tu ya walimu katika sampuli ya utafiti ndio walioonesha nia ya kuendelea kuwa walimu, wakisema mazingira magumu na maslahi duni ndio sababu kubwa za kuwavunja moyo. 

Uthibitisho mwingine wa kuwepo kwa mgomo baridi unatokana na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa. Kwa mfano katika shule za msingi, takribani nusu ya wanafunzi wamekuwa hawafaulu kwa miaka 3 sasa; huku mwaka 2011 pekee ukiwa na asilimia 46.5 ya watahiniwa waliofeli mitihani yao ya darasa la saba; na kwa sekondari wanafunzi takribani asilimia 90 walipata daraja la nne na sifuri.

Hali hii pia inadhihirishwa zaidi na uwepo wa wanafunzi zaidi ya 5,000 mwaka huu nchini walioandikishwa kujiunga na masomo ya sekondari kutokujua kusoma na kuandika.

Pia ripoti ya utafiti uliofanywa kwa niaba ya African Economic Research Consortium na Benki ya Dunia mwaka 2011 inaonesha kwamba walimu wa shule za msingi Tanzania wanafundisha kwa wastani wa masaa mawili na dakika nne tu kwa siku; kati ya masaa 5 na dakika 12 yaliyo katika ratiba ya siku moja.

RATIBA KAMILI YA UCHAGUZI NA OPERESHENI M4C NDANI YA CHADEMA

Uchaguzi ndani ya Chama na Operesheni Sangara

Ratiba mpya ya operesheni sangara baada ya maagizo ya kamati kuu iliyokaa tarehe 9 Julai 2012 ya kusimamisha uchaguzi ndani ya Chama. Kamati Kuu iliamua uchaguzi uwe unafanyika ndani ya operesheni sangara.


DATE
ENEO HUSIKA
SHUGHULI
1
04/08 2012
Kanda ya kati
Uzinduzi wa operesheni
2
05/8-19/08/ 2012
Dodoma, Singida, Iringa Manyara na morogoro
Operesherni uchaguzi ngazi ya kata.
3
19/09-30/09/2012
Makao makuu
Maandalizi
Tathimini ya operesheni
4
01/10-20/2012
Baadhi ya maeneo ya Lindi, Dsm,Pwani, Bagamoyo na Tanga
OPERESHENI
Uchaguzi ngazi ya matawi na kata
5
21/10/30/10/2012
Makao makuu
Tathimini
Maandalizi
6
01/11-20/11/2012
Kilimanjaro na Arusha
Operesheni
Uchaguzi ngazi ya matawi
7
21/11-30/11/2012
Makao makuu
Tathimini
maandalizi
8
01/12-20/12/2012
Shinyanga,Tabora na Simiyu
Operesheni na uchaguzi ngazi ya matawi na kata
9
01/01-25/01/2013
Mwanza,Geita, Mara na kagera

10
26/01-30/2013
Makao makuu
Tathimini
11
01/02-20/02.2013
Kigoma, katavi Rukwa
Operesheni na uchaguzi ndani ya chama
12
21/02-30/02/2013
Makao makuu
Tathimini ya operesheni
13
01/03-25/03/2013
Mbeya, njombe na Ruvuma
Operesheni uchaguzi
14
26/03-30/03/2013
Makao makuu
tathimini
15
01/04-25/04/2013
Zanzibar
Operesheni na uchaguzi
16
26/04-30/04/2013
Makao makuu
tathimini

Wednesday, August 1, 2012

TUWAHESHIMU WALIMU WAMETUTOA MBALI


Moja ya sababu kubwa inayochangia kurudisha nyuma maendeleo yetu, ni kwa watawala kudharau elimu na walimu wetu. Katika nchi hii, profession yoyote si kitu mbele ya mwanasiasa. katika nchi zilizoendelea, ukimuuliza mtoto unataka kuwa nani? Atakujibu kuwa anataka kuja kuwa mwalimu.

Wenzetu waalimu ni watu wa muhimu sana katika makuzi na kuelimisha jamii. Watoto, wazazi na hata serikali wanawapa heshima yao. Pia walimu wanamaslahi mazuri yanayowapa motisha, na mara nyingi wazazi huwa wanawapa hata zawadi waalimu wanaopendwa na watoto wao na kuona jinsi wanavyowaelimisha wototo wao.

Hapa kwetu miaka ya zamani ilikuwa hivyo, nakumbuka kijijini kwetu walimu, wauguzi na viongozi waliheshimika sana. Waalimu walikuwa wanasikilizwa na walikuwa wakishauri jamii mambo mbalimbali. Ila bado hadi leo ushawishi wao ni mkubwa hasa huko vijijini.

Sasa hawa wanasiasa wanaowabeza leo, wasishangae wakiona waalimu wakileta mapinduzi kwa kuwaambia wananchi hasa vijijini kuwa serikali yao haina nia njema ya kuwaletea maendeleo na kuwaelekeza cha kufanya ili kuiondoa madarakani. Mara nyingi sisi hasa waafrika tumekuwa na ulevi wa madaraka na kuamini mambo yasiyo halisi.

Inashangaza kuona kuwa, badala ya serikali kushughulikia matatizo husika, wenyewe wanataka kujiambinisha kuwa waalimu wanatumika kisiasa. Hivi kweli mtu akidai haki yake aliyoikosa miaka zaidi ya kumi, vilevile akiwa kwenye lindi la matatizo ya kupambana na maisha kwa ugumu wake. Leo unakuja kumwambia yeye si kitu na anatumika?

Bila ya hawa waalimu tusingekuwa na Madaktari, Maengineer, Wanasheria, wahasibu, wachumi, na wataalamu wengine wote. Huyu Mzee atakuwa ameongeza hasira ya waalimu dhidi ya serikali. Walifanikiwa kupandikiza chuki kwa madaktari dhidi ya wananchi, ila kwa hili la waalimu ni budi serikali ibadili namna ya kumaliza mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu sana.

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Ndugu Waandishi,

Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote  zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.

Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.

Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
  1. Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
  2. Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari  zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’  zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
  3. Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.