Rais Pierre
Nkurunzinza wa Burundi, aliyepinduliwa hivi punde toka madarakani
akiwa mazungumzoni
nchini Tanzania.
|
Meja Jenerali Godefroid
Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati
maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa
iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa
madarakani.
Meja Generali Niyombareh
amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa rais huyo
kugombea kwa awamu ya tatu.
Jenerali huyo alitimuliwa na
Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka
wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko
nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya
Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza
atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment