Dar es Salaam.
Serikali
imepoteza zaidi ya Sh362.9 bilioni kutokana na baadhi ya kashfa kubwa za
ufisadi na operesheni mbalimbali zilizoligharimu taifa tangu uhuru.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini taifa kukumbwa na kashfa mbalimbali za upotevu wa fedha
au kuanzisha mipango ambayo utekelezaji wake ulisababisha maumivu kwa wananchi
na hakuna awamu ya uongozi wa Serikali iliyokwepa hali hiyo.
Kuanzia
awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere aliyeiongoza nchi toka mwaka 1961
ilipopata uhuru hadi 1986, Rais Ali Hassan Mwinyi (1986-1995), Rais Benjamin
Mkapa (1995-2005) na Rais Jakaya Kikwete (2005-hadi sasa), kumeibuka kashfa
mbalimbali, saba zikiwa kubwa na kulitikisa taifa.
Kashfa
na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa ni pamoja na Operesheni Uhujumu
Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi
(Commodity Import Support – CIS) na Kashfa ya Rada.
Nyingine
ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na
ile ya uchotaji mabilioni katika akaunti ya Escrow.
Operesheni
Uhujumu Uchumi
Mwaka
1984 Serikali ilianzisha Operesheni Uhujumu Uchumi, iliyoongozwa na Waziri Mkuu
wa wakati huo, Edward Sokoine ili kutaifisha mali ambazo baadhi ya watu walidaiwa
kujipatia kwa njia isiyo halali.
Operesheni
hiyo ilishuhudia baadhi ya watuhumiwa wakimwaga fedha mitaani na majalalani,
huku wengine wakitupa mali kuhofia kutiwa kwenye mkono wa sheria.
Hata
hivyo, katika operesheni hiyo baadhi ya watendaji wa Serikali ambao hawakuwa
waaminifu, waliitumia nafasi hiyo vibaya kutaifisha mali za baadhi ya watu,
ambao hawakuwa wahujumu uchumi.
Zoezi
hilo lilisababisha wananchi kadhaa hasa vijijini kuwekwa ndani na wengine
kuachwa maskini baada ya kunyang’anywa mali zao ikiwamo mifugo na mashine za
kusaga nafaka, kwa kudaiwa kuwa walizipata kwa njia isiyo halali.
Mfuko
wa Commodity Import Support (CIS)
Miaka
24 baadaye yaani mwaka 2008, liliibuka sakata jingine lililokuwa na harufu
kubwa ya ufisadi wa mabilioni katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka
Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS).
Sakata
hilo liliwahusisha baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara maarufu nchini na
wizara kadhaa za Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kupitia
mfuko huo, vigogo hao walichota zaidi ya Sh200 bilioni kwa kivuli cha uagizaji
bidhaa kutoka nje ya nchi.
Mfuko
huo wa CIS, ulianzishwa katika miaka ya 1980, ambapo baadhi ya nchi wafadhili
ikiwamo Japan, zililenga kuipatia Tanzania fedha za kigeni za kununulia malighafi,
vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo, ujenzi na vingine mbalimbali.
Mpango huo ulioanzishwa na Serikali uliendelea hadi mwanzoni mwa miaka 2000,
ambapo nchi hizo wahisani ikiwamo Japan, Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia,
Norway, Uswisi, Ubelgiji, Sweden na Denmark zilikuwa zikiipatia Serikali fedha
za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.
Wizara
zilizotajwa katika orodha ya wadeni wa CIS ni pamoja na iliyokuwa ya
Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Kazi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji na
Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Tanzania Bara, wakati Zanzibar zinatajwa Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Maji.
Rada
Mwaka
2011 Serikali ilikumbwa na jinamizi la ufisadi kwa mara nyingine. Safari hii
uliibuka ufisadi wa mabilioni ya shilingi kupitia ununuzi wa rada kuukuu kutoka
Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza. Ununuzi wa rada hiyo unatajwa kutofuata
taratibu sahihi, uliligharimu taifa Sh29.5 bilioni, wakati gharama halisi
ilikuwa Sh21 bilioni.
Serikali
ya Uingereza iliamua kurudisha fedha hizo kama chenji, huku ikisisitiza kuwa
watuhumiwa wote wa hapa nchini waliohusika na ununuzi wa rada hiyo mtumba,
washitakiwe Tanzania au Uingereza kutokana na kubainika dosari kwenye ununuzi
huo.
Wakati
Uingereza ikitaka watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani, mtandao wa Wikileaks
unaosifika kwa kufichua siri za ndani ya mataifa mbalimbali duniani, ulibaini
kuwepo kwa harakati nchini za kutowafikisha mahakamani wahusika wa ufisadi huo.
EPA
Mwaka
2008 iliibuka kashfa nyingine ya wizi wa mabilioni katika Akaunti ya Malipo ya
Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ambapo vigogo kadhaa walitumia
mbinu chafu kuchota zaidi ya Sh133 bilioni katika akaunti hiyo.
Katika
wizi huo ulioitikisa nchi, wahusika walitajwa kutumia vivuli vya siasa katika
kupitisha nyaraka bila kufanyiwa uhakiki wa nyaraka hizo.
Richmond
Mwaka
2006 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani kulitokea tatizo kubwa la
uhaba wa umeme.
Hapo
ndipo Serikali ilipoanza kufanya mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kutafuta njia za dharura za kutatua tatizo hilo.
Waziri
Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa alikuwa mstari wa mbele katika mikakati hiyo
ndipo Kampuni ya Richmond Development (LLC) ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme
wa dharura na kuliuzia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanesco.
Hata
hivyo, baadaye ilibainika kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme
kama ilivyodhaniwa, badala yake kulikuwa na michezo michafu iliyofanyika kwa
masilahi ya wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Mwaka
2007, sakata hilo lilifika bungeni na aliyekuwa Spika wakati huo, Samuel Sitta
aliunda kamati iliyokuwa chini ya mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ili
kuchunguza suala hilo.
Kamati
hiyo ilichunguza sakata hilo na kutoa taarifa ilionyesha kuhusika kwa viongozi
wa juu wa Serikali akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na kusababisha
kiongozi huyo, kujiuzulu pamoja na mawaziri wawili kung’oka madarakani.
Waliong’oka
madarakani ni mawaziri wa Nishati na Madini kwa vipindi tofauti, ambao ni
Naziri Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha.
Operesheni
Tokomeza Ujangili
Operesheni
Tokomeza Ujangili iliyoanzishwa na Serikali kupambana na ujangili wa wanyama
nchini mwaka jana iliwang’oa madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao
zilielezwa kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa operesheni hiyo.
Kung’oka
kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyeeleza
kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa
mashauriano akiwa nchini Marekani.
Mawaziri
waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa shinikizo na
michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Wengine ni Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Operesheni
hiyo inadaiwa kukiuka haki za binadamu ikiwamo watu 13 na askari sita kuuawa,
utesaji wa kutisha wa watuhumiwa, ubakaji, rushwa na uporaji wa mali za
wananchi.
Akaunti ya Esrow
Wakati
kashfa ya Richmond haijasahaulika, mapema mwaka huu imeibuka kashfa ya upotevu
wa mamilioni ya fedha kwenye Akaunti ya Esrow katika Benki Kuu ya Tanzania
(BoT).
Kashfa
hiyo inayolitikisa Bunge na Serikali sasa, imetajwa kuwa ni mwendelezo wa
jinamizi la kashfa ikiwa ya saba kubwa kulikumba taifa hadi sasa.
Akaunti
hiyo iliyokuwa na zaidi ya Sh200 bilioni, ilifunguliwa wakati kukiwa kuna
mgogoro wa kisheria baini ya wabia wa zamani wa IPTL (VIP Engeneering and
Marketing na Mechmar Corporation ya Malaysia) kwa upande mmoja, Tanesco na
Independent Power Tanzania, IPT, kwa upande mwingine.
Wadau
kwenye akaunti hiyo hawakupaswa kuchukua kitu chochote hadi pale mgogoro
utakapotatuliwa. Hata hivyo, kitita hicho cha fedha kilichotwa.
Wazungumza
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Emmanuel Mallya alisema matukio ya
ufisadi yanaongezeka nchini kutokana na Serikali kushindwa kuweka bayana hatua
zinazopaswa kuchukuliwa watu wanapatikana na makosa hayo, ili iwe fundisho kwa
wengine.
Alisema
kila mara wizi wa fedha za umma unapotokea, Serikali hupata kigugumizi
kuwawajibisha wahusika, hatua inayowafanya watu wengi kuamini kushindwa kwao
kunatokana na woga wa kutekeleza azma zao.
“Hakuna
uwajibikaji kama mtu kafanya jambo fulani, kuna kulindana sana, lakini kama
wote wangechukuliwa hatua za wazi pengine ufisadi usingekuwa wa kiwango cha juu
namna hii,” alisema.
Mhadhiri
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Faraji Christoms, alishauri wenye
dhamana ya kusimamia masilahi ya taifa wanatakiwa kujitathmini upya.
Alitaja
maeneo yanayohitajika kufanyiwa tathmini kuwa ni uzalendo kwa taifa, elimu kwa
maana ya uelewa wa mambo ya kisheria, lugha za kimataifa na umakini wakati wa
majadiliano ya kimataifa na wanaposoma mikataba ya aina hiyo.
“Unakuta
mtu badala ya kutuliza akili akasoma kwa makini mkataba kabla ya kuusaini,
anaupeleka kwa msaidizi wake ukisindikizwa na memo (agizo la maandishi) “Please
read carefully for advice,” (tafadhali soma kwa makini, shauri),” alieleza
Christoms.
Alisema
katika mazingira hayo, hatima ya usalama wa mkataba huo unakuwa mikononi mwa
mwingine, tofauti na aliyepewa dhamana.
Christoms
alisema mazingira yanaonyesha kuwa wanasheria serikalini wanashindwa na
walioajiriwa kwenye kampuni za uwakili, hivyo kusababisha Serikali kupata
hasara kwa kuingia katika mikataba isiyo na masilahi kwa taifa.
Profesa
Gaudence Mpangala, wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) alisema historia ya ufisadi
nchini inamnyima mtu yeyote makini, ujasiri wa kuishauri Serikali mbinu za
kudhibiti vitendo hivyo vya rushwa.
Profesa
Mpangala alisema vitendo vya rushwa haviepukiki katika jamii, lakini Serikali
inapochukua hatua zinazothibitisha kuwa inavipiga vita, hali inakuwa shwari
tofauti na ilivyo nchini ambapo rushwa ndogo na ufisadi vimeota mizizi huku
hatua zinazochukuliwa zikiacha maswali mengi bila majibu.
Alitoa mfano wa
serikali ya awamu ya kwanza, ilivyoshughulikia rushwa iliyokuwa inaelekea
kwenye ufisadi kwa kuchukua hatua kali, chini ya hayati Edward Sokoine na
Mwalimu Nyerere ambapo waliothibitika kuhusika pamoja na adhabu ya kifungo
jela, walitakiwa kuchapwa viboko wak
No comments:
Post a Comment