Umoja wa Mataifa umesema kuwa mwanajeshi wake
mmoja wa kutunza amani ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mapigano
makali kati ya na wapiganaji wa waasi Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Wanajeshi wa serikali ya Congo |
Msemaji
wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Farhan Haq, hata hivyo hajatangaza uraia wa
wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa.
Wanajeshi
hao wa Umoja wa Mataifa walitumia ndege za helicopta kuwasukuma nyuma
wapiganaji wa M23 karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi katika
eneo hilo la Mashariki. Watu
themanini waliuawa kwenye mapigano hayo wiki iliyopita.
Mwaka
wa 2012, waasi wa M23 waliuteka mji huo kwa muda kabla ya kuondoka kufuatia
shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa. Umoja
wa Mataifa Umetuma kikosi maalum katika eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa
madini kukabiliana na waasi hao.
Wanajeshi
hao wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, wanapambana na wapiganaji hao wa waasi kwa
ushirikiano na wanajeshi wa serikali. Jeshi
hilo la Monusco limelazimika kufanya mashambulio ya anga na ardhini ili kuzuia
waasi hao wa M23 kukaribia Goma na ripoti zinasema mapigano makali yanaendelea
katika maeneo ya milima ya Kibati, takriban kilomita kumi na tano Kaskazini mwa
Goma.
Watu
wapatao laki mbili wanasemekana kuishi katika eneo hilo la Kibati. Wapiganaji
wa M23 wamesema kuwa wanajeshi wa Congo na wenzao wa Umoja wa Mataifa walifanya
mashambulio ya anga na ardhini katika maeneo wanayoyadhibiti, Kaskazini mwa
Goma.
Daktari
mmoja mjini Goma, Isaac Warwanamiza, ameliambia shirika la habari la AP kuwa
aliona miili ya watu themanini na wawili, ishirini na tatu zikiwa za wanajeshi
wa serikali. Umoja
wa Mataifa una zaidi wanajeshi elfu kumi na nane nchini Congo.
No comments:
Post a Comment