Ajali ya barabarani Kenya |
Takriban watu 41 wanadaiwa
kuuawa baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea
Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara kadhaa katika eneo la
Narok.
Polisi
wamethibitisha kuwa miongoni mwa waliouawa ni watoto wanne. Mkuu
wa polisi wilayani Narok Patterson Maelo amesema kuwa dereva wa basi hilo
alishindwa kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo
na kuanguka.
Maafisa
wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo
wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali ya
wilaya ya Narok kwa matibabu.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma risala zao za rambi
rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.
Katika
ripoti iliyochapishwa katika mtandao wake wa twitter, Rais Kenyatta ametoa amri
kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma
wanaokiuka sheria za barabarani.
No comments:
Post a Comment