FIB Tanzanian Special Forces
(part of MONUSCO) imeichukua ngome kuu ya waasi wa M23 ya Kibati (Nyirangongo
Territory - Goma, Eastern DRC).
Mizinga ya wapiganaji wetu
ilirindima na kutembeza mabomu mfululizo huku askari wetu wa miguu wakipanda
mlima ulio eneo hilo na kisha kuichukua ngome hiyo.
Yadaiwa vijana wa jeshi letu JWTZ wamepeleka mashambulizi
makali ya mabomu yaliyopelekea waasi wa kundi la M23 kuikimbia ngome yao na
hivyo kuanza kukosa mwelekeo.
Kwakweli napenda kutumia fursa hii kwa niaba yangu
binafsi, Blog hii (Maxmillian Kattikiro Blog), wadau mbalimbali na wapenda
AMANI wote kuwapongeza sana wanajeshi wetu kwa ushujaa wao na kujitolea kwao katika
kutetea haki za raia wasio na hatia wa jirani zetu wa CONGO, na Afrika kwa
ujumla.
Mungu awabariki, awalinde na kuwasimamia, huku
akiwashindia katika mapigano hayo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
na watu wake.
No comments:
Post a Comment