Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha
habari,zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini
Arusha,aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo,amepigwa
risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo,habari zinaeleza
na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA
ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye
biashara.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment