Mtoto aliyeng'olewa macho nchini Uchina |
Polisi nchini Uchina imetangaza kuwa itatoa
zawadi kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kumkamata mama mmoja
ambaye anashukiwa kumng'oa macho mvulana mwenye umri wa miaka sita.
Shambulio
hilo linasemekana kutokea tarehe 24 mwezi huu katika eneo na Fenxi, iliyoko
katika mkoa wa Shanxi.
Mvulana
huyo anasemekana alikwenda kucheza na watoto wengine lakini wazazi wake
walimpata baadaye huku macho yake yote yakiwa yamengolewa huku akivuja damu. Mvulana
huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu hospitalini.
Idara
ya polisi nchini humo imetoa zawadi ya zaidi ya dola elfu kumi na sita kwa
yeyote atakayetoa habari, kuhusu aliyehusika na shambulio hilo.
Wazazi
wa mtoto huyo wanasemekana kuwa wakulima. Mamake
amesema mtoto huyo aliwaambia kuwa wakati alipokuwa akitembea alishambuliwa na
mama mmoja ambaye hakumfahamu.
Polisi
walipata macho ya mvulana huyo karibu na eneo la tuko. Uchunguzi
wa awali umebainisha kuwa sehemu ya mboni au Cornea kwa Kiingereza ilikuwa
imengolewa, na hivyo kuashiria ulanguzi wa viungo vya kinadamu. Hata
hivyo polisi wanasema hawajatambua chanzo cha shambulio hilo.
TOA MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment