To Chat with me click here

Saturday, August 31, 2013

JESHI LA POLISI LAINGIA KATIKA KASHFA NZITO!


IGP Saidi Mwema

Gazeti la Mwananchi limeweka wazi kwamba upanga wa dhahabu aliokabidhiwa Mwema kama ishara ya kuwa mwenyekiti wa jeshi kwa kipindi cha mwaka ameshindwa kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya na iligundulika kuwa uliibiwa siku nyingi na ilibidi akabidhi upanga feki na kuahidi kwamba ataurudisha baada ya mwezi mmoja ikishindikana Tanzania itabidi itengeneze upanga mwingine wa dahabu.


Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.

Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.

Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.

IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.

Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.

Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.

Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.

Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.

Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.
  

FIB TANZANIA (SPECIAL FORCES IN CONGO) YAICHUKUA NGOME KUU YA M23!



FIB Tanzanian Special Forces (part of MONUSCO) imeichukua ngome kuu ya waasi wa M23 ya Kibati (Nyirangongo Territory - Goma, Eastern DRC).

Mizinga ya wapiganaji wetu ilirindima na kutembeza mabomu mfululizo huku askari wetu wa miguu wakipanda mlima ulio eneo hilo na kisha kuichukua ngome hiyo.

Yadaiwa vijana wa jeshi letu JWTZ wamepeleka mashambulizi makali ya mabomu yaliyopelekea waasi wa kundi la M23 kuikimbia ngome yao na hivyo kuanza kukosa mwelekeo.



Kwakweli napenda kutumia fursa hii kwa niaba yangu binafsi, Blog hii (Maxmillian Kattikiro Blog), wadau mbalimbali na wapenda AMANI wote kuwapongeza sana wanajeshi wetu kwa ushujaa wao na kujitolea kwao katika kutetea haki za raia wasio na hatia wa jirani zetu wa CONGO, na Afrika kwa ujumla. 

Mungu awabariki, awalinde na kuwasimamia, huku akiwashindia katika mapigano hayo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika na watu wake. 
 

Thursday, August 29, 2013

RAIS KAGAME, MUSEVENI NA PIERRE NKURUNZIZA LIVE KWENYE UZINDUZI WA MOMBASA PORT

Marais wa Burundi, Uganda na Rwanda, wameudhuria ufunguzi wa bandari ya Mombasa, Kenya leo! Wapo pia na wenyeji wao President Kenyatta na Bwana Rutto!

Katika matangazo yao, wamesema bandari hiyo itaunganisha Africa kibiashara hasa ikichagizwa na Ujenzi wa barabara Namanga Arusha. Hii inaashiria nini kwa mustabali wa Uchumi wa Tz ambayo 60% ya makusanyo ya kodi yanategemea bandari ya Dsm!

Museveni kahudhuria kwa kiti chake cha Uenyekiti wa EAC, ndivyo Kagame alivyomtambulisha. Pia Kagame anasema hiyo ndio faida ya Integrated East Africa Community, pia Miundombinu bora ya Bandari ya Mombasa, itaunganisha nchi zote za East Africa.

Kenyata anasema Mombasa ni Gate way of East African Business. Anasema ni manifesto ya serikali yake kuifanya bandari ya Mombasa kuwa busy and friendly port in all over East Africa coastline!

Nini hatima ya bandari ya Dsm na siasa zake? Siasa za Kenya hizo wamezindua bandari mpya leo, na wanasema Sudan, Ethiopia na Somalia watatumia bandaria hiyo pia.