Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa aliyemaliza muda wake Dr. Asha-Rose Migiro anawasili leo na
ndege ya Emirates na atapokelewa na viongozi wakuu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa waliopo Tanzania, wakiongozwa na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa
Tanzania, Dkt. Alberic Kacou.
To Chat with me click hereMonday, July 9, 2012
Chama Cha Madaktari TZ, Chawasilisha Maombi UN Ya Ulinzi Kwa Viongozi Wake:
Mchana wa leo, Jumatatu, Julai 9, 2012
Chama Cha Madaktari (MAT) kimewasilisha maombi ya ulinzi kwa Viongozi
wake na Dkt. Ulimboka (mwanachama wao) kwa Uongozi wa Umoja wa Mataifa
(UM). Nakala ya barua hiyo imepachikwa hapo juu.
Source: http://www.mjengwablog.com
Saturday, July 7, 2012
Mzee Sabodo Kuchangia CHEDEMA si tatizo - NAPE
Nape akisalimiana na viongozi wakuu wa CHADEMA hivi karibuni walipokutana kwenye msiba wa mzee Makani
"Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema. Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya
upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.
Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu
uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama
vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote
haya yamefanywa na serikali ya CCM.
Sasa kama serikali ya CCM imefanya hivyo, cha ajabu hapa kwa
mwanachama wake kufanya hivyo ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha
watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!
Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!!
Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa
itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni
nini?!
Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!", Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika taarifa yake..
HII SIYO HOJA YA KAA CHINI .......
Kutokana na mlundikano wa mambo katika bunge letu kiasi kwamba Mheshimiwa sana, Spika wa Bunge letu kuonekana kuelemewa na mambo hayo, je anaweza kusaidi na kusimamizi kwa umakini hoja zinazokidhi matakwa ya watanzania kimaendeleo? - comment.
Asante ya katuni kutoka kwa mdau Said Michael.
Asante ya katuni kutoka kwa mdau Said Michael.
JK AMPONGEZA ASKOFU PROTASE RUGAMBWA WA JIMBO KATOLIKI LA KIGOMA
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za
pongezi Askofu Protase Rugambwa wa Jimbo Katoliki la Kigoma (pichani), kwa
kuteuliwa kwake na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa XVI
kuwa Katibu Mwambata (Adjunct) wa Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwa ajili
ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, Roma.
“Ninakupongeza kwa
dhati kabisa kwa kuteuliwa kwako katika wadhifa huo mkubwa nikitambua kwamba
uteuzi huo unatokana na imani kubwa aliyo nayo kwako Papa Benedict wa XVI
kutokana na uwezo wako mkubwa kiuongozi na unyenyekevu ulionao kwa watu wako, hivyo nakutakia kila
la kheri na mafanikio makubwa katika kuutumikia wadhifa wako mpya”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za
pongezi.
Aidha Rais Kikwete
amesema anafarijika sana na uteuzi wa Askofu Protase Rugambwa kwa sababu uteuzin huo
umeliletea heshimakubwa Taifa letu nakwa mara nyingine umethibitisha jinsi
viongozi mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wa dini walivyo na imani na uwezo
wa watu wetu katika Nyanja za uongozi.
Askofu Protase Rugambwa
amewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu kumaliza masomo yake ya Teolojia huko
Roma nchini Italia, ambayo hatimaye mwaka 2008 yalimwezesha kuteuliwa na Papa
Benedicti wa XIV kuwa Askofu wa Jimbo la Kigoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar-es-Salaam.
JK AMPONGEZA BABA ASKOFU TARCISIUS NGALALEKUMTWA KWA KUTEULIWA KUWA RAIS WA TEC
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amempongeza Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa (PICHANI) kwa kuteuliwa kwake
kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akichukua nafasi ya
Baba Askofu Yuda Tadei Rwaich aliyemaliza muda wake.
“Nimefarijika
sana na uteuzi wako kushika wadhifa huo muhimu hasa kutokana na imani kubwa
waliyonayo Maaskofu kuhusiana na uwezo wako katika kukiongoza chombo hicho
muhimu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake.
“Ninatambua
na kuthamini mchango mkubwa ambao, kwa muda mrefu sasa, Kanisa Katoliki
limekuwa likuutoa kwa maendeleo ya nchi yetu, hasa katika Nyanja za huduma za
jamii.
Aidha
uhusiano mzurpi kati ya serikali ninayoiongoza na Kanisa Katoliki unaendelea
kunitia moyo, hivyo ninakuhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya nne itaendeleza
nakuimarisha uhusiano huu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla”,
amesema na kusisitiza Rais katika salamu zake za pongezi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar-es-Salaam.
Thursday, July 5, 2012
UTATA WATANDA NCHI ANAKOTIBIWA DR. ULIMBOKA
WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven
Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika
hospitali moja ya huko Ujerumani. Habari zilizotufikia jana
zimeeleza kuwa Dk. Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa
muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu
yake sasa.
Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk. Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
“Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari. Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”
Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk. Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.
Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”
“Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk. Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”
Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe, alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.
Alisisitiza kuwa Dk. Ulimboka yupo Afrika Kusini anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.
Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk. Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk. Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.
Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.
Rafiki asimulia mkasa
Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.
Dk Deogratius alisema jana kwamba siku ya tukio walikuwa wametokea kwenye msiba wa ndugu wa mwalimu wao Profesa Yongolo na baada ya msiba walikwenda Viwanja vya Leaders saa moja usiku kuangalia taarifa ya habari na mambo mengine.
Huko walikutana na madaktari wengine na ilipofika saa 4:00 usiku, Dk Ulimboka aliwaambia kwamba kuna jamaa alikuwa akimtafuta hivyo angependa kwenda kukutana naye.
“Tukamwuliza anamtafutia nini? Akatueleza kuwa kwa siku tatu huyo jamaa anamtafuta. Wenzangu wakasema asiende mwenyewe na mimi ndiyo nikamsindikiza. Mara ya kwanza huyo jamaa alisema anaitwa Abeid na alisema yuko Sterio, tukaenda huko hatukumkuta tukaenda Hugo hatukumkuta lakini baadaye tukakutana naye maeneo ya Barabara ya Tunis karibu na Ofisi za Ultimate Security.”
Dk Deogratius alisema wakati wakiendelea na mazungumzo, Abeid alikuwa akitaka kujua nini kinachotakiwa ili kutatua mgogoro uliopo wa madaktari.
“Wakati tunamalizia mazungumzo nilikwenda msalani, niliporudi Abeid alikuwa akizungumza na simu kila wakati, tuliendelea na mazungumzo hadi tukamaliza na kuanza kuagana,” alisema.
Alisema wakati wakiagana bado walikuwa wamekaa katika viti pamoja na Abeid... “Ghafla kuna watu walifika na kusema kuwa wanamtaka Dk Ulimboka. Walimchukua na kwenda naye katika gari. Walikuwa watano, walikuwa ‘giant’ (miili mikubwa) na ‘very skilled’ ( wenye uzoefu) wakamchukua Dk Ulimboka wakaenda naye kwenye gari,” alisema Dk Deogratius.
Alisema wakati huo Abeid alikuwa anakimbia hivyo akamkimbilia ili ampe namba yake ya simu ambayo ingemsaidia kwa mawasiliano.
“Alinipa namba yake nikampigia muda huohuo lakini nilipokuja kumpigia tena sikumpata na mpaka leo hapatikani,” alisema.
Alisema baada ya tukio hilo alimpigia mke wa Dk Ulimboka na kumweleza na pia alipiga simu polisi kuwaeleza.
“Nilikwenda polisi kutoa maelezo na nikawapa namba zangu za simu zote ili wanipigie kama watapata chochote, lakini mtu wa kwanza kunipigia asubuhi (kesho yake) alikuwa Juma Mgaza (aliyemwokota Dk Ulimboka) ambaye alinieleza kuwa kuna rafiki yangu amempa hiyo namba na kwamba yuko hoi amepigwa.”
Alisema baada ya kupata simu hiyo aliwasiliana na watetezi wa haki za binadamu ambao walimtaka waende pamoja na kwamba walipokuwa njiani kuelekea Kituo cha Polisi Bunju alipigiwa simu na polisi wa kituo hicho.
Kutokana na hali hiyo aliomba iundwe tume huru ikijumuisha wanasheria, madaktari na watu wengine ili ukweli ujulikane.
Upelelezi wa Polisi
Kamanda wa Polisi

Tuesday, July 3, 2012
Mbeki :Reclaim Africa’s Position in the World
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe akiwa na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini alipomtembelea Nyumbani Kwake, Midrand - Afrika Kusini.
"Nilipata fursa ya kumtembelea Rais Mstaafu wa Afrika Kusini ndugu Thabo
Mbeki nyumbani kwake Midrand, Afrika Kusini-Tulizungumza masuala
mbalimbali kuhusu Bara la Afrika, masuala ya Uongozi katika AU, mgogoro
wa Sudan na Libya na nafsi yake katika siasa za Ulimwengu".
BUNGE LACHAFUKA KUPIGWA ULIMBOKA
Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, hali ndani ya bunge jana jioni
ilichafuka, baada ya mwenyekiti wa bunge, kushishwa kabisa kuongoza
kikao hicho kufuatia kuzuka kwa malumbano makali baada ya Mkuu wa mkoa
wa Iringa, Stella Manyanya kukituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kuwa vinara wa mgomo wa madaktari.
Manyanya alisema kuwa, CHADEMA wamebainika kuchochea mgogoro huo, hali
iliyomfanya Mbunge wa Ubungo kusimama na kuomba mwongozo akimtaka
Manyanya kuthibitisha ama kukanusha tuhuma hizo.
Lakini katika hali ya kushangaza, Mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu
Mchemba alisimama na kunukuu hotuba ya kambi ya upinzani, ambayo
ilitamka bayana kuwa inaunga mkono madai ya watumishi wa serikali, na
kwamba kwa kauli hiyo inadhihirisha bayana kuwa ndio wakuu wa mgomo huo.
Badala ya kutoa mwongozo, Mabumba hakumtaka Manyanya kukanusha ama
kuthibitisha alimruhusu Mchemba kuendelea kurusha makombora mazito dhidi
ya CHADEMA, safari hii akidai kuwa ni vimbelembele kutoa matamshi ya
kulaani kupigwa kwa Ulimboka huku, wakimwacha mmoja wa viongozi wake
bila kumhudumia wala kumjulia hali.
Katika kujichanganya kwa wabunge hao wa CCM, wakati Mchemba akidai
kuwa CHADEMA ndio wachocheaji wakubwa wa mgogoro huo kwa kuwatumia
madaktari, mwenzake Manyanya alitoa hoja safari hii akidai kuwa, ndio
waliohusika na tukio la kumvamia na kumteka na kisha kumpiga Dk.
Ulimboka.
Hata pale Mnyika aliposimama na kuomba tena mwongozo wa mwenyekiti,
huku akiweka bayana jinsi inavyoelezwa ushiriki wa maafisa wa polisi, na
hata Dk. Ulimboka mwenyewe kuwataja wengine kwa majina, alimtaka
mchangiaji kuthibitisha ushiriki wa CHADEMA kumjeruhi ama siyo afute
kauli yake.
Lakini kwa mara nyingine tena, Mabumba hakumtaka Manyanya wala Mchemba
kuthibitisha kauli ama kufuta kama inavyofanywa kwa wabunge wa
upinzani, badala yake alimruhusu mkuu huyo wa mkoa wa Iringa kuendelea
na mchango wake bila kufuta kauli wala kuithibitisha.
Kushindwa huko kwa waziwazi kwa Mwwenyekiti wa kikao hicho cha bunge,
kuliwachefua wabunge wengi wa upinzani, huku wale wa CCM wakionekana
kufurahia jambo hilo.
MADAKTARI BINGWA WAMJIBU KIKWETE
AGIZO la Rais Jakaya Kikwete kuwataka madaktari wanaoendelea na mgomo
kuacha kazi limechukua sura mpya baada ya madaktari bingwa ambao awali
hawakuhusika kabisa na mgomo huo, kutoa tamko wakimtaka kiongozi huyo wa
nchi kuwatimua wao kwanza kabla ya wale wa ngazi ya chini. Badala yake, madaktari bingwa ambao walitangaza kujiunga na wenzao
juzi, baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Dk. Steven Ulimboka,
walisema wataendelea na mgomo wao hadi hapo serikali itakapowarejesha
kazini madaktari na madaktari wanafunzi wote waliofukuzwa.
Akitoa tamko la madaktari bingwa waliokutana kwa dharura jana na
kamati ya jumuiya ya madaktari kujadili hotuba ya rais Kikwete, kiongozi
wa mabingwa hao Dk. Catherine Mng’ong’o alisema huo ni msimamo wa
madaktari wenzake, huku akitaka kufunguliwa kwa meza ya majadiliano ya
dhati yenye nia ya kumaliza mgogoro wao.
“Madaktari bingwa hatuwezi kufanya kazi bila madaktari wa chini yetu…
kama serikali imedhamiria kuwafukuza kazi hawa na interns (waliopo
kwenye mafunzo ya vitendo) ianze na sisi.
“Tuko tayari kufukuzwa iwapo madai yetu ya msingi hayatatekelezwa na
kama kuondoka waanze kutufukuza sisi kwanza,” alisema Dk. Mng’ong’o
baada ya kumalizika kwa kikao cha madaktari bingwa kilichoketi kwa zaidi
ya saa tano kwenye viunga vya hospitali hiyo.
Alisema hata wao hawana sababu ya kuendelea kufanya kazi katika
mazingira magumu na kuwaona Watanzania wakifa kwa kukosa vifaatiba na
dawa. Dk. Mng’ong’o alisema madaktari hapa nchini wamefanya kazi katika
mazingira magumu kwa muda mrefu hivyo wakati wa kubadili hali hiyo
umefika na kuwasaidia Watanzania maskini wanaotibiwa kwenye hospitali
hizo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dk. Godbless Charles alihoji sababu za kuwepo kwa taarifa tofauti kuhusu ongezeko la mishahara wakati waliishauri serikali kuwa wazi kuhusu nyongeza hiyo.
“Kumekua na majibu tofauti mfano Waziri wa Afya na UStawi wa Jamii aliliambia Bunge kwamba nyongeza ya mishahara ni asilimia 15. Hotuba ya rais Kikwete inasema nyongeza hiyo ni asilimia 20 wakati ripoti ya wataalam iliyokutana na kamati ya Waziri Mkuu ilipendekeza asilimia 25 je, nia ya serikali iko wapi?
“Wakati viongozi wa serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana ripoti ya ufafanuzi wa madai na hoja za madaktari iliyotokana na majadiliano ambapo tulikuwa wajumbe hatukutoa pendekezo lolote juu ya ongezeko la mshahara,” alisema Dk. Godbless.
Alisema tangu kuanza kwa mgogoro kati ya madaktari na serikali jumla ya vikao sita viliketi kati ya hivyo vikao vinne vilijadili juu ya uboreshaji wa huduma za afya kwa watanzania. “Ni masikitiko yetu kuwa ripoti ya ufafanuzi wa hoja na madai yetu iliyotolewa Juni 31 mwaka huu, taarifa ya waziri wa afya, taarifa ya waziri mkuu ndani ya Bunge na hotuba ya rais haikuzungumzia kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa watanzania,” alisisitiza Dk. Godbless.
Katika hotuba yake kwa wananchi rais Kikwete aliwataka madaktari wote waliogoma kuchakazi kwa kuwa viwango vikubwa vya mishahara wanaoitaka serikali haiwezi kuilipa.
- Waomba kukutana na Rais

Monday, July 2, 2012
HATIMAYE DR. ULIMBOKA APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU
Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi
ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa
kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana
alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya
kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari
kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko
wa ubongo.
Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege
aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na
wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi
walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo
lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja
huo.
DR. ULIMBOKA AITESA SERIKALI
SIKU chache baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ahmed
Msangi, kudaiwa kuhusika kwenye sakata la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, imeelezwa kuwa ofisa
huyo amewekewa ulinzi mkali.
Habari za ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa ofisa huyo anaishi kwa mashaka
kutokana na tuhuma nzito aliyotupiwa, hatua iliyowafanya wakuu wake kumpa
walinzi wawili wa kulinda usalama wake wakati huu ambapo uchunguzi unaendelea
chini ya tume maalumu iliyoundwa.
“Issue ya Dk. Ulimboka imemweka pabaya afande Msangi, anaishi kwa hofu sana
hadi kufikia hatua ya kupewa walinzi wawili,” kilieleza chanzo chetu cha
habari.
Hata hivyo, pamoja na kukiri kusikia tuhuma hizo ambazo amezikana, Msangi
ameviambia vyanzo vyetu vya habari kuwa, yeye hana hofu kwa kuwa anajua
hajafanya wala kuhusika kwa namna moja ama nyingine na tukio la Ulimboka.
Alikanusha kupewa ulinzi, ingawa vyanzo vyetu vya habari vilishuhudia kwa
siku mbili akiwa ameambatana na watu wengine wawili kila alipokwenda, ingawa
alikiri kuwa ni askari wake na kwamba hilo ni jambo la kawaida.Kwa mujibu wa kanuni za kazi za polisi, Kamanda wa Polisi wa mkoa ama wa
Kanda Maalumu ndiye tu anayepewa ulinzi binafsi, lakini si mkuu wa upelelezi wa
mkoa.
JK, serikali imtese Ulimboka kwa lipi?
Rais Jakaya Kikwete, ameeleza kushangazwa kwake na tuhuma zilizotolewa na
baadhi ya madaktari na wana harakati kwamba serikali inahusika kumteka na
kumpiga kikatili mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari, Steven Ulimboka.
Katika hotuba yake jana kwa Watanzania, Kikwete pamoja na kuelezea
masikitiko yake makubwa na kuhuzunishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa
Dk. Steven Ulimboka usiku wa Juni, 26, 2012, alidai kushangazwa na tuhuma
kwamba serikali inahusika na ukatili huo, akisema haoni sababu ya msingi ya
kufanya hivyo, ikizingatiwa kuwa ndiye aliyekuwa kiungo muhimu baina ya
serikali na madaktari.
Kikwete alisema ingawa ni ukweli kwamba Dk. Ulimboka hakuwa mtumishi wa
serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano hayo na pia kulikuwa na
rai ya kutaka asiwepo, bado ndiye aliyeamuru aachwe aendelee kuwapo maadam
madaktari wenzake wamemuamini na anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao
wenyewe walioajiriwa na serikali.
Aliongeza kuwa kutokana na mwenendo wa mazungumzo ulivyokuwa ukiendelea,
hakukuwa na sababu za serikali kufikia hatua ya kumdhuru Dk. Ulimboka.“Kwa nini serikali imdhuru Dk. Ulimboka? Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi
na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa
ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana
shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa,” alisema.
SERIKALI YAOMBA MADAKTARI NJE YA NCHI
• Bilioni 200 zatengwa kuwalipa
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi
huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri
kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya
Kikwete.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa
na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote
zilizofanywa kuboresha maslahi yao.
Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa
ajili ya kuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza
limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na
zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari
wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.
Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi
rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba
kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.
Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za
matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi
ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika
kurejeshwa kazini kwa masharti makali.
Hata hivyo, uamuzi wa serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.
Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini
walikwama baada ya Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa
suala hilo liko mahakamani.
Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na
serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema
serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna
kesi mahakamani.
“Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo
lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo
mahakamani?” alihoji Dk. Kigwang’ala.
Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia
mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliwafukuza kazi
madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na
mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.
Jeshi lachukua nafasi za madaktari
Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeanza
kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu kwa
wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini. Juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua
kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wastaafu
na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma ya matibabu kwa
wagonjwa.
Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe katika mahojiano maalum na
gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo,
walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali
Kuu ya Jeshi Lugalo Kikosi ya 521, Mgulani na ile ya Kikosi cha
Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma
hiyo bila vikwazo.
“Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa
asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo
hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika
hospitali zetu labda kwa asilimia 90.
Mgawe alisema madaktari wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na
watu wake, hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua kutosita kwenda
katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya
daktari kugoma.
MAONI YA MBUNGE WA UBUNGO KUHUSU HOTUBA YA MH. DKT. JAKAYA KIKWETE RAIS WA TANZANIA KWA WANANCHI TAREHE 30 JUNI 2012
Jana tarehe 1 Julai 2012 kumesambazwa katika mitandao ya kijamii na
baadhi ya vyombo vya habari hotuba ya Mh. Dkt. Jakaya Kikwete Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi inayotajwa kutolewa tarehe
30 Juni 2012.
Kufuatia hotuba hiyo na kufuatia mwito kutoka wachangiaji wa mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kutaka maoni yangu kuhusu hotuba husika, naomba nichukue fursa hii kutoa maoni kwa nafasi yangu ya ubunge kuhusu hotuba tajwa kama ifuatavyo:
Hotuba hiyo ya Rais imeibua mjadala na masuala ambayo yanahitaji kujadiliwa bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge unaoendelea hivyo, serikali isiendelee tena kutumia kisingizio cha mahakama kulizua bunge kujadili masuala husika wakati yenyewe inayajadili na kuyatolea maelezo na maelekezo pamoja na kuchukua hatua hususani kuhusu suala la mgomo wa madaktari.
Hotuba hiyo ya Rais ukindoa suala la usafirishaji haramu wa watu nchini inaelekea kuwa ndiyo kauli ya Serikali ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kwamba ingetolewa bungeni lakini baadaye serikali ikasema haitatoa kauli. Uamuzi wa Serikali kuitoa kauli hiyo kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge wasijadili hotuba husika na pia wasitimize wajibu wa kikatiba wa ibara 63 (2) wa kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.
Hivyo, Ofisi ya Rais na Ikulu wanapaswa kutoa maelezo kwa umma sababu za Rais kutolihutubia taifa tarehe 30 Juni 2012 kama ilivyotangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kielectroniki na badala yake hotuba ya Rais kusambazwa tarehe 1 Julai 2012 kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari na iwapo masuala ya hotuba hiyo kuhusu mgomo wa madaktari ndiyo yale ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikusudia kuyaeleza bungeni.
Aidha, kwa kuwa bunge litajadili mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kuanzia kesho tarehe 2 Julai 2012 na kuendelea ni muhimu wabunge wakajadili pia masuala ambayo Rais ameyaeleza kwa taifa na kutimiza wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 (2) wa kuishauri na kuisimamia serikali.
Kuhusu Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini

Ni vizuri hotuba ya Rais imeeleza wazi kwamba tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa Tanzania kwa kuwa kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwa na ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu katika taifa letu kupitia mipaka ya mikoa mbalimbali hapa nchini. Kwa mbinu yoyote ile ambayo imetumika, matukio haya yanaashiria kwamba mipaka yetu haipo salama kwa kuwa kama malori na vyombo vingine vya usafiri vyenye watu wasio na hati za kuingilia nchini wanaweza kuingia kwa wingi kwa nyakati mbalimbali tafsiri yake ni kwamba nchi iko kwenye hatari ya kuingiziwa pia vitu vingine haramu ikiwemo madawa ya kulevya na silaha hali ambayo ni tishio kwa usalama wa nchi na maisha ya wananchi. Ni vizuri Rais amekutana tarehe 27 Juni 2012 na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzungumzia tukio hilo; hata hivyo, zaidi ya kuwapongeza vyombo vya dola kwa kazi nzuri ya kudhibiti shughuli za biashara haramu, nilitarajia kwamba Rais kwa mujibu wa mamlaka yake ya ibara ya 33 (2) ya mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu angeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu udhaifu uliojitokeza na kuagiza hatua kuchukuliwa kwa walishindwa kudhibiti hali hiyo katika mipaka ambayo biashara haramu ya usafirishaji wa watu inapitia. Izingatiwe kwamba mianya hii katika mipaka yetu ina athari pana sio katika suala hili tu bali pia katika usalama wa maisha ya wananchi kama ilivyo katika mikoa ya Kigoma, Kagera na kwingineko ambapo uhai wa wananchi na mali zao uko mashakani kutokana na uvamizi toka kwa wahamiaji haramu. Aidha, athari za hali hiyo zimejitokeza katika usambazaji wa chakula toka kwenye hifadhi ya taifa ambapo pamoja na Serikali kutumia zaidi ya bilioni 27 kusambaza mahindi na nafaka nyinginezo bei za bidhaa hizo katika Soko la Dar es salaam ikiwemo katika Jimbo la Ubungo hazikushuka kutokana na vyakula hivyo kutoroshwa na kuuzwa nje ya nchi kutokana na udhaifu katika ulinzi kwenye mipaka.
Hivyo, ni muhimu wabunge wakati wa mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais wataka kuongezeka kwa uwajibikaji na usimamizi wa utawala wa sheria ili kudumisha amani nchini.
Hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa ni pamoja na bunge kuisimamia serikali kuhakikisha idara ya usalama wa taifa inafanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kuvisaidia vyombo vingine vya dola kulinda mipaka ya nchi na pia matatizo ya maslahi katika vyombo vya ulinzi na usalama yanatatuliwa ili vyombo husika viweze kufanya kazi bila baadhi ya maofisa wake kujihusisha na vitendo vya ufisadi na kuruhusu biashara haramu za aina mbalimbali.
Kuhusu Mgomo wa Madaktari
Kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa; hotuba ya Rais imeendeleza kauli za upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kuhusu mgogoro huo bila taifa kupewa fursa ya kupata maelezo na vielezo vya upande wa pili; hivyo kuwa serikali imetoa kauli yake hadharani badala ya bungeni au mahakamani, ni muhimu pia taarifa ya kamati ya bunge ya huduma za jamii iliyoshughulia suala hilo na kukutana na pande zote mbili itoe taarifa yake bungeni na kwa umma.
Katika hotuba yake Rais amewaeleza kwa kiwango kikubwa wananchi namna ambavyo madaktari wanasababisha mahangaiko kwa wagonjwa wengi na kusababisha vifo kwa wengine lakini hakueleza kabisa mchango wa serikali katika kusababisha hali hiyo. Hivyo, kwa kuwa pande zote mbili zinachangia katika athari zinazoikumba nchi na wananchi kutokana na mgomo; ni muhimu chombo cha tatu kikaingilia kati kuwezesha ufumbuzi kupatikana na chombo hicho ni bunge ambalo ndilo lenye wajibu wa kuisimamia serikali. Jitihada za kuwalazimisha madaktari kurejea kazini bila majadiliano ya pande mbili mbele ya chombo cha kuisimamia serikali kushughulikia chanzo cha mgogoro huo zinaweza kuleta ufumbuzi wa muda mfupi na athari za muda mrefu.
Ieleweke kwamba hata madaktari wakisitisha mgomo wa wazi kutokana na amri ya mahakama na agizo la Rais, migogoro katika ya serikali na watumishi wa umma wenye kusababisha migomo baridi ya chinichini ina madhara ya muda mrefu kwa taifa.
Mathalani, kutokana na migomo baridi na huduma mbovu katika sekta ya afya wananchi wa kawaida wamekuwa wakifa kutokana na magonjwa yanayotibika.
Migomo ya chini kwa chini ya walimu na mazingira mabovu yamekuwa yakisababisha kudidimia kwa elimu katika shule za umma; mwanafunzi aliyehitimu masomo yake bila kujua kusoma na kuandika hana tofauti na mgonjwa anayekufa kwa kukosa huduma.
Hali hii ya kugoma kusiko kwa wazi imeenza kujipenyeza mpaka kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuachia mianya ufisadi na kushindwa kusimamia utawala wa sheria kama ivyodhihirika kwa kuongezeka kwa vitendo vya biashara haramu katika taifa letu.
Rais amewaeleza wananchi kuwa kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari na kwamba katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa na pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. Hata hivyo, katika masuala matano yaliyobaki, Rais hakueleza kwa wananchi nini ambacho serikali ilikuwa tayari kutoa kwa kila madai na kwa kiasi gani badala yake ameonyesha tu kwa ujumla kwamba madai hayo hayatekelezi.
Aidha, kufuatia hotuba hii ya Rais Madaktari nao wana wajibu wa kuueleza umma msingi wa madai yao na kwa kiwango gani walikuwa tayari kushuka kutoka katika madai yao ya awali, kinyume na hayo itaonekana kwamba madaktari waliingia katika majadiliano wakiwa na msimamo wa kutaka madai yao pekee ndiyo yakubaliwe wakati ufumbuzi wa mgogoro wa pande mbili hupatikana kwa win win (give and take).
Ni vizuri ikafahamika kwamba katika majadiliano, pande zote mbili huwa na mapendekezo yake; hivyo upo uwezekano kwamba yapo madai ambayo madaktari wameyatoa ambayo serikali haina uwezo wa kuyatimiza kwa kiwango walivyopendekeza na yapo ambayo serikali imeyakataa wakati ambao ina uwezo wa kuyatekeleza hata ikiwa kwa kiwango pungufu ya kile kilichopendekezwa na madaktari.
Suluhu katika mgogoro kama huo ambao kila upande una mapendekezo yake linapaswa kufanywa na vyombo vya usuluhishi; hata hivyo kuwa suala hili linahusu mgawanyo wa rasilimali za nchi na bajeti ya serikali, chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ni bunge.
Na kwa kuwa kamati ya bunge ya huduma za jamii ilikutana na pande mbili, ilikuwa muhimu kwa serikali kabla ya kupeleka shauri mahakamani kurejesha kwamba suala husika bungeni ambalo ndilo lenye wajibu wa kupendekeza vipaumbele vya mpango wa serikali na ndilo lenye kuidhinisha bajeti ya matumizi ya serikali.
Uamuzi wa serikali kukimbilia mahakamani kabla ya majadiliano ya bunge umechangia katika kusababisha mgomo wa madaktari, hivyo ushauri wangu kwa Rais Kikwete ni kwa serikali kufuta kesi iliyoko mahakamani ili bunge lipewe fursa ya kujadili ripoti yake kamati yake na kupitisha maazimio ya kuwezesha suluhu kati ya serikali na madaktari.
Mahakama iwe ni hatua ya mwisho baada ya mihimili miwili muhimu ya serikali na bunge kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea wenye athari kwa nchi na maisha ya wananchi.
Rais Kikwete ameeleza taifa kwamba Serikali imeongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12; hata hivyo serikali inapaswa pia kulieleza taifa namna ambavyo kiwango hicho cha fedha kinapungua ukiweka kizio (factor) cha kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumumo wa bei ukilinganisha mwaka 2005 na 2012.
Ukweli ni kwamba bajeti ya Sekta ya Afya bado ni ndogo kwa kuwa serikali haijatimiza bado azimio la kutenga asilimia 15 kwa ajili ya bajeti ya afya pia, hata kiwango hicho cha ongezeko la fedha hakijaleta matokeo ya kutosha kutokana na matumizi kuelekezwa kwenye baadhi ya maeneo yasiyokuwa ya kipaumbele na kuwa na utegemezi wa kiwango kikubwa cha fedha za wahisani ambazo kwa mwaka huo wa 2011/2012 aliourejea Rais Kikwete hakikutolewa kwa kiwango kilichoahidiwa. Hivyo, Rais Kikwete awezeshe kuongezwa kwa fedha za ndani kwenye bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Katika madai mengine Rais Kikwete ameeleza kwamba pande mbili zilifikia makubaliano nusu nusu, hali ambayo inaashiria kwamba madaktari wana hoja ambazo zinahitaji majadiliano hivyo, ni muhimu bunge likapewa nafasi ya kujadili kuweza kuwakilisha pande zote mbili za serikali na madaktari kuhusu nini kinawezekana na nini hakiwezekani ili kulinusuru taifa na mgogoro unaoendelea.
Rais Kikwete ametumia kwa kiwango kikubwa madai ya madaktari ya ongezeko la mshahara kujaribu kuwachonganisha wananchi na madaktari kwa kuwa na madai yasiyotekelezeka. Hata hivyo, ni muhimu ikafahamika kwamba sio madaktari pekee ambao wana mgogoro na mwajiri wao yaani serikali kuhusu kiwango cha mshahara bali pia watumishi wengine wa umma ikiwemo walimu.
Nyongeza iliyotolewa na serikali ya kati ya asilimia 15 na 20 kwenye mwaka wa fedha 2012/2013 ni tofauti na ahadi ambazo serikali imekuwa ikitoa kwa wafanyakazi za kuongeza mishahara na kupunguza kodi katika mishahara. Rais Kikwete na serikali warejee maoni na mapendekezo ya kambi rasmi ya upinzani kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na 2012/2013 kuhusu nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma na vyanzo mbadala vya mapato vya kuongeza kwa ajili ya kuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji. Uwiano wa sasa wa matumizi ya mishahara kuwa asilimia 48 ya bajeti badala ya uwiano mzuri wa asilimia 35 kuwa mishahara na na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa; ni matokeo ya udhaifu wa serikali katika kupanua vyanzo vya mapato, kupunguza matumizi ya kawaida yasiyo ya lazima na kuongeza fedha katika miradi ya maendeleo hali ambayo Rais Kikwete kuliwezesha bunge kuisimamia serikali na kuirekebisha.
Kuhusu Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Rais Kikwete ameeleza wananchi kuwa ameelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane; hata hivyo kauli hii inaashiria kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi kuunda jopo la kuchunguza.
Nilitarajia Rais Kikwete kwa kutambua uwepo wa madai ya polisi kutuhumiwa kuhusika katika jaribio la mauji ya Dr Ulimboka angetangaza kuunda tume huru ya uchunguzi au walau angeongeza nguvu katika jopo la uchunguzi lililoundwa kwa kuunda timu ya maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama na usalama pamoja na wadau wengine kutoka taasisi huru.
Rais Kikwete anapaswa kutumia madaraka yake kwa mujibu wa katiba kuunda tume huru ambayo inadhihirisha kwa vitendo kwamba watuhumiwa hawajichunguzi wenyewe na kuwezesha matokeo ya uchunguzi kuaminika.
Narudia kuwasihi madaktari kuendelea kuokoa maisha ya wananchi katika kipindi hiki kigumu lakini wakati huo huo Rais Kikwete aiongoze serikali kuepusha athari zaidi katika sekta ya afya ya kuwa na mgogoro na madaktari kwa kuliwezesha bunge kujadili suala hili na kulipatia ufumbuzi ikiwemo kupitia nyongeza ya bajeti ya Wizara ya Afya. Nimemwandikia barua Spika Anna Makinda akiwa ni mkuu bunge kama muhimili mmojawapo wa dola kuweza kuchukua hatua stahili, naomba pande zote zizingatie maoni yanayotolewa na wabunge kwa niaba ya wananchi kwa maslahi ya taifa.
Maoni haya yametolewa Jana tarehe 1 Julai 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Bungeni-Dodoma
Subscribe to:
Posts (Atom)