To Chat with me click here

Wednesday, July 3, 2013

ZIARA YA RAIS WA MAREKANI BARRACK OBAMA NCHINI TANZANIA KATIKA PICHA!


Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto zao, wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam siku ya tar. 1. Nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
Rais. Jakaya Kikwete akiwa na Mgeni wake Rais wa Marekeni Baraka Hussein Obama, huku picha ya juu ikionesha wake za marais hao nao wakiwa pamoja.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam siku ya tar. 1. Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani Spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. A. Kificho muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais. Barrack Obama wa Marekani akipokea salamu ya heshima kutoka kwa mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Brig. Gen. Davis Mwamunyange, baada ya kutambulishwa kwake na mwenyeji wake Rais. Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais. Barrack Obama na Mwenyeji wake wakipokea heshima na kupigiwa nyimbo za mataifa yao, baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais. Kikwete.
Rais. Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na wanajeshi wa JWTZ.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Kwa habari zaidi  katika Picha akiwa Ikulu ...





































Rais. Barrack Obama akipanda mti wa kumbukumbu Ikulu Dar-Es-Salaam, baada ya mapokezi na mwenyeji wake Rais. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, akimsindikiza mwenyeji wake Rais wa Marekani Barrack Obama, baada ya mapokezi kabambe Ikulu,Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment