William and Kate show off their son to the world - but they are still undecided about the name for the Prince of Cambridge. |
Ujumbe wa heri njema umeendelea
kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa
tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.
Mwanamfalme William na mkewe Kate
,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa
kwanza Jumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na takriban
kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini hajapewa
jina.
Katika taarifa fupi William,amesema
wana furaha isiyo na kifani. Baadaye leo jeshi la Uingereza
linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40
hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.
Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa
mwanamfalme huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na
moja ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la
Buckingham, zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na
habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa
mara ya kwanza.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron,
alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana kwa
Uingereza.
Naye wawiri mkuu wa Australia, Kevin
Rudd, alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola,
huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William baada ya
kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.
No comments:
Post a Comment